1.1. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Nov 2, 2016, 10:49 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


 1. "Ki' imetumiwaje katika sentensi: Meni alipokuja alinipata nikifyeka.
  1. kuonyesha hali ya masharti
  2. kuonyesha hali ya kukanusha
  3. kuonyesha hali ya kuendelea
  4. kuonyesha hali ya udogo
 2. Ni sentensi ipi sahihi?
  1. ndizi lililoletwa ni langu
  2. miti zilizopandwa zimeota
  3. zulia iliyonunuliwa ni zuri
  4. wema unaozungumziwa ni huu
 3. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni sehemu ipi iliyo tofauti na zingine?
  1. paja
  2. kiganja
  3. pafu
  4. goti
 4. Polepole, vibaya, Alasiri, Njiani, ni
  1. vielezi
  2. vivumishi
  3. nomino
  4. viwakilishi
 5. Methali inayotoa funzo kuwa: Jambo linaloonekana zito kwa mwingine laweza kuwa rahisi kwako ni
  1. bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi
  2. mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi
  3. kila mwamba ngoma ngozi huvutia kwake
  4. ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno
 6. Sentensi "asingalikwenda kwake asubuhi asingalimkuta" ina maana kuwa:
  1. hakuenda kwake asubuhi lakini alimkuta
  2. alienda kwake asubuhi lakini hakumkuta
  3. alienda kwake asubuhi na akamkuta
  4. hakuenda kwake asubuhi wala hakumkuta
 7. Ni maneno yapi ambayo yote ni viunganishi?
  1. ila, ingawa, lakini, maadamu
  2. huyo, hao, ovyo, na
  3. ila, lakini, vizuri, wima
  4. ingawa, isipokuwa, zuri, safi
 8. Kivumishi cha sifa kutokana na kitenzi angaa Ni:
  1. angaza
  2. angazia
  3. angavu
  4. angalau
 9. 7/8 kwa maneno ni:
  1. subui nane
  2. thumuni saba
  3. subui
  4. thumuni
 10. Kisawe cha neno barobaro ni:
  1. banati
  2. kijana
  3. mvulana
  4. shaibu
 11. Nomino habari iko katika ngeli ya:
  1. U-ZI
  2. I-I
  3. U-I
  4. I-ZI
 12. TANO ni kwa CHOKAA. KITITA ni kwa
  1. pesa
  2. funguo
  3. ndizi
  4. ngozi
 13. Haya ni maumbo gani?
  kiswahili kcpe topical questions
  1. pembe tatu, mche, duara
  2. pia, mcheduara, nusuduara
  3. pia, mchemraba, mcheduara
  4. pemebe tatu, pia, nusuduara
 14. Chagua usemi halisi ufaao wa:    
Bahati alisema kuwa angeenda nyumbani kupumzika
  1. "Nimeenda nyumbani kupumzika", bahati alisema
  2. "niende nyumbani kupumzika", bahati alisema
  3. "Nitaenda nyumbani kupumzika", bahati alisema
  4. "nilienda nyumbani kupumzika', bahati alisema
 1. Yapange maneno yafuatayo kulingana na jinsi yanavyotokea katika kamusi:
(i) bandika    (ii) beua    (iii) birika    (iv) baidika
  1. (i) (iv) (ii) (iii)
  2. (iv) (ii) (iii) (i)
  3. (ii) (i) (iii) (iv)
  4. (iv) (i) (ii) (iii)

1.1. Fasihi Sehemu Kwanza - Majibu [you need to sign in first and to sign in, you must be a member]

1.0 Fasihi Sehemu Nunge - Maswali

1.2. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Pili - Maswali


Nyuma

Lalamika kwa majibu yasiyo sahihi; tuma ujumbe kwa sales@manyamfranchise.com


kifungu cha kujaza pengo