1.2. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:02 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


 1. Salamu "alamsiki" hujibiaje?
  1. katika
  2. bila
  3. kwa
  4. kwenye
 2.  Chagua usemi halisi wa
  mwalimu aliwauliza kama wangeandika insha siku hiyo jioni.
  1. "Mtaandika insha kesho jioni?" Mwalimu aliwauliza
  2. "Kesho jioni mngeandika insha?" Mwalimu aliwauliza
  3. "Mtaandika insha leo jioni?" mwalimu aliwauliza.
  4. Leo jioni mngeandika insha?" mwalimu aliwauliza.
 3. Jina wanaloitana ndugu wa kike na wa kiume ni
  1. Umbu
  2. Somo
  3. Mnuna
  4. Kaka
 4. Maana ya methali
  "Ganda la muwa la jana chungu kuona kivuno" ni:-
  1. jambo ambalo unaliona rahisi kwako kwa mwenzako huenda likawa gumu
  2. kitu unachokiona duni kwako, huenda kikawa na manufaa kwa mtu mwingine
  3. haifai kudharau kitu chako duni kwa kutamani cha mwenzako
  4. haifai kuwadharau watu waliokusaidia hapo awali, huenda ukawahitaji baadaye.
 5. Polepole, vibaya, alasiri, njiani ni:
  1. vivumishi
  2. nimino
  3. viwakilishi
  4. vielezi
 6. "Ki" imetumiwaje katika sentensi.
  mwesi alipokuja alinipata nikifyeka
  1. kuonyesha hali ya masharti
  2. kuonyesha hali ya kuendelea
  3. kuonyesha hali ya kukanusha
  4. kuonyesha hali ya udogo
 7. 7/8 kwa maneno ni:
  1. subui nane
  2. subui
  3. thumuni saba
  4. thumuni
 8. Nomino habari iko katika ngeli ya:
  1. U-ZI
  2. I-I
  3. U-I
  4. I-ZI
 9. Haya ni maumbo gani?
  kiswahili std 8 topical questions
  1. pembe tatu, mche, duara
  2. pia, mchemraba, mcheduara
  3. pia, mcheduara, nusuduara
  4. pembe tatu, pia, nusuduara
 10. Chagua wingi wa sentensi:
  hukujua kuwa ningewatembelea?
  1. hawakujua kuwa tungewatembelea?
  2. hamkujua kuwa tunge watembelea?
  3. hamkujua kuwa ningewatembelea?
  4. hawakujua kuwa ningewatembelea?
 11. Chagua sentensi yenye "na" ya kuonyesha mtendaji
  1. Jane ameandikiwa barua na Rehema
  2. Akida na Anaja ni wanafunzi wazuri
  3. Tamaa na ubinafsi ni chanzo cha wovu
  4. Ninunulie matunda na mboga
 12. Kukanusha kwa sentensi
  Maria ameingia darasani akanipata ni:-
  1. Maria hajaingia darasani wala hajanipata
  2. Maria hakuingia darasani wala hakunipata
  3. Maria haingii darasani wala hanipati
  4. Maria ameingia darasani wala hakunipata
 13. Panga vifungu vufuatavyo kuunda sentensi yenye maana kamili
  1. Yanayohusu maisha yao
  2. Vijana wa hirimu
  3. Huwa na mazungumzo
  4. Kuhusu mambo
  1.  (iv), (iii), (i), (ii)
  2. (ii), (iv), (iii), (i)
  3. (i), (ii), (iii), (iv)
  4. (ii), (iii), (iv), (i)
 14. Chagua sentensi anayoonyesha kwa ya matumizi
  1. amealikwa harusini kwa Hamisi
  2. ameenda kwa haraka
  3. alienda ulaya kwa ndege
  4. tulikula wali kwa mchuzi
 15. Tofauti ya maana kati ya wanne na wa nne ni:
  1. wanne ni idadi ya jumla na wa nne ni idadi kamili katika orodha
  2. Wanne ni kuonyesha idadi kamili na wa nne ni anayechukua nafasi ya nne katika orodha
  3. Wanne ni idadi kamili na wa nne ni idadi katika orodha
  4. Wanne ni kuonyesha sifa na wa nne ni kuonyesha idadi
kifungu cha kujaza pengo