1.3. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Tatu - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:04 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1.     Kitenzi  kwa kielezi ni kama nomino kwa:-
 1. Kivumishi
 2. kihusishi
 3. Kiunganishi    
 4. kiashiria
2.     Chagua sentensi yenye kivumishi ‘ji’ cha kuonyesha ‘binafsi’.
 1. Jino langu laniuma sana.
 2. Baada ya kudhurika alijifinya sikio.
 3. Hakuna awezaye kupigana na jitu lile.
 4. Matatu hutumika kwenye usafirishaji wa abiria.
3.     Makao ya konokono huitwaje
 1. Tundu
 2. Kombe
 3. Gae
 4. Gogo
4.     Kamilisha sentensi kwa usanifu:Darasa letu lina wanafunzi:-
 1. Kumi na nane
 2. Wakumi na nane
 3. Kumi na wanane
 4. Wakumi na wanane
5.     Ni orodha ipi yenye maneno yanayohusiana na seremala
 1. Mbao, msumeno, timazi, nyundo
 2. Msumari, randa, sepetu, podo
 3. Timazi, pima-maji, nyundo, msumari
 4. Keekee, utepe, randa, msumeno
6.     Kisawe cha ‘sebule’ ni:
 1. Ukumbi
 2. Maskani
 3. Msala
 4. Kiwanda
7.     Tegua kitendawili: Maiti anasema huku waliombeba wamenyamaza.
 1. Nzi na kinyesi
 2. Chungu na mafiga
 3. Moto na kuni
 4. Ulimi na meno
8.     Jaza pengo kwa kutumia kihisishi.
“_______Juma yuko wapi?” Baba alishangaa. 
 1. Kwani
 2. Huyo
 3. Do!
 4. Hujui
9.     Tumia kitenzi kilichopigwa mstari uunde nomino mwafaka. Mwalimu wetu aliingia darasani akaanza kutusaili
 1. Sala
 2. Masuala
 3. Maswali
 4. Mawasiliano
10.   Chagua sentensi iliyoakifishwa barabara.
 1. Abiria aliuliza ndege ingetua saa ngapi
 2. Maradhi ya Ukimwi ni hatari sana: yanafisha
 3. Nunua; sukari, majani-chai, mkate nasiagi
 4. Wambua na kamau wameelekea mombasa
11.   Majira ya baridi kali huitwaje?
 1. Kipupwe
 2. Masika
 3. Mapukutiko
 4. Matlai
12.   Ipi ni tashbihi?
 1. Mtihani huu ni jiwe
 2. Mwanariadha ametimka kama risasi
 3. Sote tumetulia tuli
 4. Nani amevuta mkia?
13.  Tumia viambishi mwafaka ukamilishe sentensi
 1. Ze, zo, zi
 2. Ye, so, ya
 3. Ye, yo, i
 4. Ye, so,tu
14.  ‘Kanga’ ni aina ya ndege. ‘Kanga’ pia ni______
 1. Mtu apakiaye abioria garini
 2. Ile hali ya kuchoma chakula kwennye mafuta
 3. Neno lenye maana sawa na ‘tibu’
 4. Shuka ya kujitandia kiunoni
15.   Chagua kitenzi chenye kiambishi _tamati
 1. Kufurahi
 2. Wanasoma
 3. Keti
 4. Ondoka
kifungu cha kujaza pengo