1.4. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:05 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1   Andika kinyume.

Mtwana amemaliza chakula kitamu.

A  mtwana amemuaga chakula kitamu.

B  kijakazi  ametema chakula kichungu.

C  kijakazi ametema chakula chapwa.

D  kijakazi ametapika chakula chapwa.

2    Chagua usemi taarifa ufaao:

“Ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho”mama alisema.

A  Mama alidai kwamba ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho.

B  Mama alimwambia kwamba akimwiita mapema atampeka sokoni kesho.

C  Mama alisema kuwa angemwita mapema angempeleleka sokoni siku iliyotangulia.

D  Mama alisema kuwa angemwita mapema angempeleka sokoni siku iliyofuata.

 3  Chagua sentensi yenye vivumishi

A Mama ameanika nguo nje ya nyumba.

A  Yule aliimba vuzuri mno akatuzwa

C Tunatarajia wawe hapa wakati wowote

D  Walimu wengi walishiriki katika mgomo huo

4  Ni sentensi ipi ambayo imetumia –kwa- ya kuonyesha kusudi.

A Nimefika kwa kutaka kumwona mkurugenzi.

B  Yeye aliadhibiwa kwa rafiki yake

C Timu hizo zilifungana mabao mawili kwa nunge

D  Wazee kwa vijana walihudhuria karamu hiyo

5  Ki- katika sentensi. Alikuwa akicheza kitoto;imetumika kuonyesha .

A wakati,kielezi

B kielezi ,masharti

C ngeli,wakati

D masharti,ngeli

 6  Tegua  kitendawili:janga laniandama usiku kucha

A mwezi

B nyota

C ngurumo

D kunguni

7 Chagua sentensi yenye maelezo  yaliyo sahihi kabsaa.

A ! hutumika kuonyesha neno halikukamilishwa katika nafasi fulani.

B .  : hutumika kuonyesha maneno yenye hisia.

C   ; hutumika kutenganisha kauli mbili zilizo na uhusiano wa karibu

D  ?hutumika kuonyesha mwisho wa sentensi.

8. Ni sentensi  gani iliyo na maana ya kumhadaa mtu ama kumpa sifa asizostahili

A kumpa nyama ya ulimi

B kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa

C kumwaga mtama mbele ya kuku wengi

D kuzama katika bahali ya luja

9  chagua sentesi yenye taswira jozi

A Kamau na ndugu yake  weusi kama makaa.

B Yeye ni duma katika mbio za nyika.

C Ana maneno mengi kuliko chiriku.

D Wao ni maji na mafuta tangu walipozomeana

10 neno ambalo limetumia silabi chengamano

A uzalishaji

B utulivu

C kikapu

B umuhimu

11   andika kwa wingi: gazeti lake limetafunwa na mbuzi

A  Magazeti yao yametafunwa na mbuzi

B  Magazeti yao yametafunwa na mabuzi

C  Gazeti zao zimetafunwa na mbuzi

D Gazeti zao zimetafunwa  na mabuzi

12   chagua sentensi iliyo katika hali ya mazoea

A   alipatikana akitumia dawa za kulevya.

B   ameenda sokoni bila kwaheri wala tahayuri

C   wao huenda kanisani kila siku ya jumapili.

D   anapenda sana kuandamana na watu wakubwa

13  kipindi cha miaka kumi huitwa?

A  kikwi

B  korija

C  mwongo

D  karne

14  Siku hizi bei ya maembe ni afadhali. Hivi ni kusema bei__

A  imepungua

B  inapanda

C  haijabadilika

D  haijulikani

15  Chagua orodha inayoonyesha vimelea pekee.

A  mbung’o,kunguni,kiroboto,papasi,funza.

B  kitumbi,chafuo,bombwe,kitungule

C  dama , kilebu ,  nge,kisuse,kimatu

D  chawa,kimatu,chafuo,kiroboto

kifungu cha kujaza pengo