1.6. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:08 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


Kitoka nambari 1-10 jibu maswali kulingana na maagizo

1. Ndege mwenyeuwezo wa kuiga usemi wa binadamu ni yupi?
A. kiweto
B. kasuku
C. tumbili
D. paka

Kutoka 2-3 jibu vitendawili

2. Hachagui chifu wala mjumbe______
A. utelezi
B. Ulimi
C. Maisha
D. barabara
3. Babu geuka geuka____________
A. ndege
B. siafu
C. kinyonga
D. ng'ombe

Kutoka 4-5 jibu Methali

4. Akutupaye hajali _______
A.Wewe
B. mambo
C.watu
D. atakapoanguka
5. Ngano ina ncha __________
A.kumi
B.saba
C.moja
D.Nane
6. Andika kwa wingi: katika katiba ,mshindi wa urais atatakiwa kupata asilimia 50 – na moja juu ili kutangazwa mshindi .
A.katika katiba ,washindi wa urais watatakiwa kupata asilimia 50- na moja juu ili kutangazwa washindi .
B.katika katiba ,lishindi wa maurais atatakiwa kupata asilimia 50-na moja juu ili kutangazwa washindi.
C. katika makatiba ,washindi wa maurais watatakiwa kupata maasilimia 50- na mamamoja majuu ili kutangazwa washindi .
D.katika makatiba washindi wa ueais watatakiwa kupata asilimia 50 na moja juu ili kutangazwa washindi

Kutoka 7-8, Unganisha kuunda sentensi

7.
i)rais siku 21 kabla ya muhula wa rais aliye mamlakani
ii)wakenya
iii)kumalizika ,ikiwa katiba kielelezo itaidhinishwa
iv)watakuwa wakimchagua
A. I,ii,iii,iv
B. iv,iii,ii,i
C. ii,iv,i,iii
D. ii,iv,I,iii
8.
i)ambapo aliwataka wakazi kuendelea kunyunyiza maji mashambani ili kukubali kiangazi
ii)Bw. Wafwa alisema hayo baada
iii)wilayani Ganze
iv)ya kukagua hali ya mabwawa
A. I,iv,ii,iii
B. ii,iv,iii,i
C. Iv,ii,iii,i
D. Ii,iv,I,iii
9. Ni lipi ambayo sio moja ya kundi hili?
A. Siagi
B. Mawere
C. Mtama
D. Wimbi
10. Kiswahili ni kinyume cha lugha gani ?
A. Kiborana
B. Kihindi
C. Kikuyu
D. Kimombo
kifungu cha kujaza pengo