1.7. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:09 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Andika kinyume: Mtwana amemeza chakula kitamu
a. Mtwana amemwaga chakula kitamu.
b. Kijakazi ametema chakula kichungu.
c. Kijakazi ametema chakula chapwa.
d. Kijakazi ametabika chakula chapwa
2. Chagua usemi taarifa ufaao:
“ Ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho, ” mama alisema.
a. Mama alidai kwamba ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho
b. Mama alimwambia kuwa akimwita mapemaatampeleka sokoni kesho
c. Mama alisema kuwa akimwita mapema angempkeleka sokoni siku iliyotangulia
d. mama alisema kuwa angemwita mapema angempeleka sokoni siku iliyofuata
3. Chagua sentensi yenye vivumishi.
a. Mama ameanika nguo nje ya nyumba.
b. Yulew aliimba vizuri mno akatuzwa.
c. Tunatarajia wawe hapa wakati wowote.
d. Walimu wengi walishiriki katika mgomo huo.
4. Ni sentensi ipi ambayo imetumia –kwa- ya kuonyesha kusudi.
a. Nimefika kwa kutaka kumwona mkurugenzi.
b. Yeye aliadhibiwa kwa rafiki yake.
c. Timu hizo zilifungana mabao mawili kwa nunge.
d. Wazee kwa vijana walihudhuria karamu yangu.
5. Ki-katika sentensi.Alikuwa akicheza kitoto: imetumika kuonyesha.
a. wakati, kielezi
b. kielezi, masharti
c. ngeli, wakati
d. masharti, ngeli
6. Tegua kitendawili. Janga laniandama usiku kucha.
a. Mwezi
b. Nyota
c. Ngurumo
d. kunguni
7. Chagua sentensi yenye maelezo yaliyo sahihi kabisa.
a. ! hutumika kuonyesha nenohalikukamilishwa katika nafasi fulani
b. : hutumika kuonyesha maneno yenye hisia.
c. : hutumika kutenganisha kauli mbili zilizona uhusiano wa karibu
d. ? hutumika kuonyesha mwisho wa sentensi
8. Ni semi gani iliyo na maana ya kumhadaa mtu au kumpa sifa asizozistahili.
a. Kumpa nyama ya ulimi
b. Kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
c. Kumwaga mtama
d. kuzama katika bahari ya luja
9. Chagua sentensi yenye taswira jozi.
a. Kamau na ndugu zake ni weusi kama makaa
b. Yeye ni duma katika mbio za nyika.
c. Ana meno mengi kuliko chiriku.
d. Wao ni maji na mafuta tangu walipozomeana.
10. Chagua neon ambalo limetumia silabi chengamano
a. Kikapu
b. Umuhimu
c. Uzalishaji
d. utulivu
11. Andika kwa wingi. Gazeti lake limetafunwa na mbuzi.
a. Magazeti yao yametafunwa na mbuzi.
b. Magazeti yao yametafunwa na mabuzi.
c. Gazeti zao zimetafunwa na mbuzi.
d. Gazeti zao zimetafunwa na mabuzi.
12. Chagua sentensi iliyo katika hali ya mazoea.
a. Alipatikanaakitumia dawa za kulevya.
b. Ameenda sokoni bila kwaheri wala tahayuri.
c. Wao huenda kanisani kila siku yaJumapili.
d. Anapenda sana kuandamana na watu wakubwa.
13. Kipindi cha miaka kumi huitwa?
a. Kikwi
b. Korija
c. Mwongo
d. karne
14. siku hizi bei ya maembe ni afadhali. Hivi ni kusema bei____
a. imepungua
b. inapanda
c. haijabadilika
d. haijulikani
15. chagua orodha inayoonyesha vimelea pekee.
a. Mbung’o, kunguni, kiroboto, papasi, funza
b. Kitumbi, chafuo, bombwe, kitungule
c. Dama, kilebu, nge, kisuse, kimatu,
d. Chawa, kimatu, chafuo, kiroboto
kifungu cha kujaza pengo