1.8. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Nane - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:10 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Maneno yaliyopigiwa mstari ni___ Mageti haya mapya yatawekwa vizuri yale makuukuu yatachomwa kabisa
A. Kiashiria,kiashiria,kivumishi
B. Kivumishi ,kiwakilishi,kielezi
C. Kivumishi,kiashiria,kivumishi
D. Kiwakilishi ,kivumushi,kitenzi
2. Mdudu mwenye mbawa nne wa rangi ya kahawia na apendaye kukaa mahali penye giza na kuruka usiku ni ___
A. Nondo
B. Kiwavi
C. Koyoko
D. Kumbi kumbi
3. Ni methali ipi iliyo tofauti na nyingine ?
A. Jungu kuu halikosi ukoko
B. Jifya moja haliinjiki chungu
C. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo
D. Kidole kimoja hakivunji chawa
4. Igeuze sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa .”Nikihitaji msaada wako nitakufahamisha ,”akaniahidi
A. Ameniahidi kwamba akihitaji msaada wangu atanifaamisha
B. Alimwahidi kuwa angemfaamisha iwapo anghitaji msaada wake .
C. Aliniahidi kuwa angenifahamisha iwapo angehitaji msaada wangu .
D. Alimwahidi kwamba angemfahamisha iwapo akihitaji msaada wake.
5. Wingi na ukubwa wa sentensi ifuatayo ni ___.Mwizi amemwibia mama Yule mwavuli wake .
A. Wezi wamewaibia akina mama wale miavuli yao
B. Majizi yameyaibia majimama yale majiavuli yao
C. Majizi yamewaibia majimama yale miaviuli yao
D. Vijizi vimeviibia vijimama vile vijaavuli vyao .
6. Tunaposema kutupa jongoo na mti wake ; tunamaanisha ____
A. Kusahau na kuwacha kabisa
B. Kuona uzito wa mambo
C. Kumbuka mambo kwa wakati
D. Wafaa kuchukua mambo kwa uzito
7. Ni sentensi ipi iliyo na ‘kwa’ iliyotumika kama kihusishi ?
A. Alisafiri kwa ndege
B. Alienda kwa mwalimu mkuu
C. Alifungwa kwa kuiba
D. Tulikula wali kwa nyama
8. Chagua kundi lenye maneno ya viarifa :
A. Vizuri,polepole ,kishamba ,mno
B. Cheza,imba,kula,soma
C. Viatu ,darasa,nguo,nyumba
D. Bilahi,ehee,lahaula,alhamdulahi
9. Tegua kitendawili Baba akipiga mbizi huibuka na ndevu nyeupe
A. Muwa
B. Kinu
C. Mbegu
D. Mwiko
10. Chagua kinyume cha sentensi hii ,musa alisifiwa kwa utiifu wake
A. Musa hakusifiwa kwa utiifu wake
B. Musa alikashifiwa kwa utundu wake
C. Musa alikashifiwa kwa ukaidi wake
D. Musa hakukashifiwa kwa ukaidi wake
11. “Ungejizatiti jino ukucha ungefua dafu “ sentensi hii inamaanisha
A. Ulifua dafu kwa bidii zako
B. Ulijizatiti lakini hukufaulu
C. Ulitia bidii kwa mapana marefu ukafua dafu kwa mapana na mafupi
D. Hukufua dafu kwa kutojizatiti
12. Chaguya sentensi iliyoandikwa kwa kutumia ‘O’ rejeshi ya awali kwenye kitenzi
A. Mtu anayekuja pale ametoka tanga
B. Kiota tuonacho hapa niche ndege aitwaye chiriku
C. Nguo auzazo sasa ni maridadi
D. Kiti kiletwacho ni cha babu
13. Chagua sentensi ambayo ni muungano sahihi wa hizi ,Mburukenge aliingia uwanjani .Mburukenge aliwafadhaisha wanafunzi
A. mburukenge aliingia uwanjani na kuwafadhaisha wanafunzi
B. mburukenge aliingia uwanjani kwa kuwafadjaisha wanafunzi
C. mburukenge aliingia uwanjani lakini aliwafadhaisha wanafunzi
D. mburukenge aliingia uwanjani kwani aliwafadjaisha wanafunzi
14. Zawadi apewayo mtu aliye pata kitu kilichopotea huitwa
A. Rubani
B. Fola
C. Kiangazamacho
D. karo
15. Rangi inayofanana na utando wa maziwa wenye mafuta yanyoweza kutengenezwa samli au huitwa ____
A. Rangi ya waridi
B. Feruzi
C. Malai
D. zafarani
kifungu cha kujaza pengo