1.5. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:06 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1.       Kanusha : Amekula na amestarehe
a.       Hakula na akastarehe
b.      Hakula wala hajastarehe
c.       Hajala na hajastarehe
d.      Hajala wala hajastarehe
2.       Dadaye mamaye ni
a.       Halati
b.      Ami
c.       Shangazi
d.      Mama mdogo
3.       Msemo huu,”Tupa jongoo na mti wake,”una maana gani?
a.       Kukumbuka haya mambo kila wakati
b.      Kumsengenya baada ya kuondoka
c.       Kuyasahau na kuyaacha kabisa
d.      Chukua mambo mazito mtu asiyoweza
4.       Ni sayari gani iliyo na miezi mingi?
a.       Dunia
b.      Mshtarii
c.       Zaibaki
d.      utairidi
5.       Subui mbili mara dufu ni
a.       Subui nne
b.      Mbili kwa kumi na nne
c.       Nne kwa kumi na nne
d.      Kumi na nne
6.       Wingi wa ukubwa wa: Mti huu umekauka n
a.       Mti hii imekauka
b.      Jiti hili limekauka
c.       Majiti haya yamekauka
d.      Vijiti hivi vimekauka
7.       Ni saw kusema:________wa mahindi
a.       Chane
b.      Kidani
c.       Kichala
d.      ufefe
8.       Neno kiweto liko katika ngeli ya
a.       Ki-vi
b.      A-wa
c.       U-zi
d.      Li- ya
9.       Ni sentensi lipi iliyo sahihi
a.       Maji yameijaza mito
b.      Maji yameyajaza mito
c.       Maji imejaza mito
d.      Maji ume jaza mito
10.   Mkato wa wifi zake ni
a.       Wifio
b.      Wifiwe
c.       Wifize
d.      wifizo
11.   Kikuba nip ambo ambalo huvaliwa
a.       Mguuni
b.      Shingoni
c.       Sikioni
d.      kichwani
12.   chagua sentensi sahihi
a.       angekuja
b.      asingekuja hangenipata
c.       angalikuja angenipata
d.      asingalikuja asingepata
13.   Onyesha kitenzi ambacho hakiwezi kuwa katika kauli ya kutendua
a.       Chana
b.      Ziba
c.       Omba
d.      choma
14.   C hagua neno lisilofaa kati ya haya
a.       Surupwenye
b.      Kiamshakinywa
c.       Batamzinga
d.      mkemwenza
15.   Onyango aliokota cheti kilichopotea kwa hivyo alilipwa
a.       Kiinua mgongo
b.      Kiingilio
c.       Kiokozi
d.      ada 
kifungu cha kujaza pengo