1.0. Fasihi Kitengo cha Kwanza Sehemu Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 28, 2015, 7:26 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Andika kinyume: Mtwana amemeza chakula kitamu
A. Mtwana amemwaga chakula kitamu
B. Kijakazi ametema chakula kichungu
C. Kijakazi ametema chakula chapwa
D. Kijakazi ametapika chakula chapwa
2. Chagua usemi taarifa ufaao: “ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho” mama alisema.
A. Mama alidai kwamba ukiniita mapema nitakupeleka sokoni kesho
B. Mama alimwambia kuwa akimwita mapema atampeleka sokoni kesho
C. Mama alisema kuwa angemwita mapema angempeleka sokoni siku iliyotangulia
D. Mama alisema kuwa angemwita mapema angempeleka sokoni siku iliyofuata
3. Chagua sentensi yenye vivumishi
A. Mama ameanika nguo nje ya nyumba
B. Yule aliimba vizuri mno akatuzwa
C. Tunatarajia wawe hapa wakati wowote
D. Walimu wengi walishiriki katika mgomo huo
4. Ni sentensi ipi ambayo imetumia –kwa-ya kounyesha kusudi
A. Nimefika kwa kutaka kumwona mkurugenzi
B. Yeye aliadhibiwa kwa rafiki yake
C. Timu hizo zilifungana mabao mawili kwa nunge
D. Wazee kwa vijana walihudhuria karamu yangu
5. Ki-katika sentensi. Alikuwa akicheza kitoto; imetumika kuonyesha
A. Wakati, kielezi
B. Kielezi, masharti
C. Ngeli, wakati
D. Masharti, ngeli
6. Tegua kitendawili. Janga laniandama usiku kucha
A. Mwezi
B. Nyota
C. Ngurumo
D. Kunguni
7. Chagua sentensi yenye maelezo yaliyo sahihi kabisa
A. ! hutumika kuonyesha neno halikukamilishwa katika nafasi fulani
B. : hutumika kuonyesha maneno yenye hisia
C. ; hutumika kutenganisha kauli mbili zilizo na uhusiano wa karibu
D. ? hutumika kuonyesha mwisho wa sentensi
8. Ni semi gani iliyo na maana ya kumhadaa mtu au kumpa sifa asizostahili
A. Kumpa nyama ya ulimi
B. Kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa
C. Kumwaga mtama mbele ya kuku wengi
D. Kuzama katika bahari ya luja
9. Chagua sentensi yenye taswira jozi
A. Kamau ni weusi kama makaa
B. Yeye ni duma katika mbio za nyika
C. Ana maneno mengi kuliko chiriku
D. Wao ni maji na mafuta tangu walipozomeana
10. Chagua neno ambalo limetumia silabi changamano
A. Kikapu
B. Umuhimu
C. Uzalishaji
D. Utulivu
11. Andika kwa wingi. Gazeti lake limetafunwa na buzi
A. Magazeti yao yametafunwa na mbuzi
B. Magazeti yao yametafunwa na mabuzi
C. Gazeti zao zimetafunwa na mbuzi
D. Gazeti zao zimetafunwa na mabuzi
12. Chagua sentensi iliyo katika hali mazoea
A. Alipatikana akitumia dawa za kulevya
B. Ameenda sokoni bila kwaheri wala tahayuri
C. Wao huenda kanisani kila siku ya Jumapili
D. Anapenda sana kuandamana na watu wakubwa
13. Kipindi cha miaka kumi huitwa?
A. Kikwi
B. Korija
C. Mwongo
D. Karne
14. Siku hizi bei ya maembe ni afadhali. Hivi ni kusema bei
A. Imepungua
B. Inapanda
C. Haijabadilika
D. Haijulikani
15. Chagua orodha inayoonyesha vimelea pekee
A. Mbung’o, kunguni, kiroboto, papasi, funza
B. Kitumbi, chafuo, bombwe, kitungule
C. Dama, kilebu, nge, kisuse, kimatu
D. Chawa, kimatu, chafuo, kiroboto

1.0 Fasihi Sehemu Nunge - Majibu [you need to sign in first and to sign in, you must be a member]


Nyuma

Lalamika kwa majibu yasiyo sahihi; tuma ujumbe kwa sales@manyamfranchise.com

kifungu cha kujaza pengo