2.0. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 8:14 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Neno tama lina maana sawa na
a. Hatia
b. Uchoyo
c. Shauku
d. wivu
2. Kamilisha methali hii: Mtaka hana
a. kisu
b. mkatiwa
c. lake
d. kinyongo
3. Mtoto huyu amekuwa mkubwa (ukubwa)
a. Matoto hawa wamekuwa kubwa
b. Toto hili limekuwa kubwa
c. Kijana amekuwa mkubwa
d. Kijitoto hiki kimekuwa kikubwa
4. Ki ya wakati inapatikana katika sentensi
a. Kidole kinaniuma
b. Alikuwa akila ugali
c. Kilema ameshinda mashindano
d. Kile kitu kizuri
5. Mfano wa kiashiria hapa ni
a. Ndivyo
b. Ambaye
c. Hiyo
d. bali
6. Kinyume cha sentensi, ajuza analala
a. Mkongwe anaamka
b. Bibi anaota
c. Sahibu anaamka
d. Shaibu anaamka
7. Tano ni kwa chokaa. Kitita ni kwa
a. Pesa
b. Funguo
c. Ndizi
d. ngozi
8. Yapange maneno yafuatayo kulingana na jinsi yanavyotokea katika kamusi
i. Bandika
ii.Beua
iii.Birika
iv.Baidika
a. i, iv, ii, iii
b. iv, ii, iii, i
c. ii, i, iii, iv
d. iv, i, ii, iii
9. Akifisha: Mama aliwauliza kwa nini hamkumkaribisha mgeni
a. Mama aliwauliza, “kwa nini hamkumkaribisha mgeni?”
b. Mama aliwauliza, “kwa nini hamkumkaribisha mgeni”
c. Mama aliwauliza “kwa nini hamkumkaribisha mgeni?”
d. Mama aliwauliza ‘kwa nini hamkumkaribisha mgeni”
10. Ni kundi lipi halilingani?
a. Mibalungi, mindazi, matomoko, mifenesi
b. Keekee, tezo, patasi, jiriwa
c. Kishaufu, bali, kikuba, kikero
d. Shore, mbayumbayu, heroe, keng’ende
11. Kanusha sentensi ifuatayo: Mwanasheria angekuwa kortini angeonekana
a. Mwanasheria angekuwa kortini asingeonekana
b. Mwanasheria asingelikuwa kortini asingelionekana
c. Mwanasheria hangekuwa kortini asingeonekana
d. Mwanasheria asingekuwa kortini asingeonekana
12. Chagua kiunganishi kifaacho kukamilisha sentensi hii: Juma amefaulu mtihani wake ____hajapata shule
a. Ndio
b. Ila
c. Pia
d. Basi
13. Ni maneno yapi ambayo yote ni vivumishi vya sifa? ___
a. Huyu, hapa, kile, hicho
b. Wewe, yeye, sisi, wao
c. Sana, kivivu, kingwana, haraka
d. Maahiri, duni, tele, bora
14. Haya ni maumbo gani?
pia, mcheduara, nusuduara, mstatili 
a. Pembe tatu, mche, duara, mstatili
b. Pia, mcheduara, nusuduara, mstatili
c. Pia, mchemraba, mcheduara, mstatili
d. Pemba tatu, pia, nusuduara, mstatili
15. Kisawe cha neno barobaro ni
a. Banati
b. Kijana
c. Mvuluna
d. Shaibu
kiswahili revision papers