2.4. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 21, 2015, 9:40 PM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. 13.07%___
a. ASILIMIA KUMI NA TATU NUKTA SABA
b. ASILIMIA KUMI NA TATU NA SUFURI SABA
c. Asilimia kumi na tatu nukta sufuri
d. Asilimia kumi na tatu nukta sufuri saba
2. Ipi sahihi ?
a. Bumba la nyuki
b. Buda la noti
c. Kigaro cha askari
d. Kaumi ya watu
3. Ni nini maana ya: Johana ana mkono mrefu
a. Ni mwoga
b. Si mwizi
c. Ana uwezo
d. Ni mnyonge
4. Umoja wa nyanya kali ni
a. Nyanya mkali
b. Mnyanya mkali
c. Nyanya kikali
d. Nyanya kali
5. Ipi ni dhahania ?
a. Uzi
b. Wema
c. Uteo
d. wembe
6. katika matwana hiyo ,kulikuwa na abiria thelathini.ushuri mbili walikuwa watoto wanaume walikuwa watoto nao wanaume walikuwa sita. Je, wanawake walikuwa wangapi?
a. 6
b. 18
c. 30
d. 12
7. Nywele zilizo kati ta pua na mdomo wa juu katika uso wa mtuni zinaitwa
a. Ndevu
b. Kionjamchuzi
c. Masharubu
d. mianzi
8. KANUSHA: mtu aliyeongea ninamjua
a. Mtu aongeaye simjui
b. Mtu asiyeongea ninamjua
c. Mtu ambaye hakuongea simjui
d. Mtu asiyaongea simjui
9. Ni sentensi ipi ina kielezi?
a. Ana vitabu vizuri
b. Ana vyoo vyake
c. Tulicheza vizuri
d. Kalamu hii nzuri
10. Kutokakana na kitenzi kujua, tunapata nomino ipi?
a. Kuelewa
b. Kujuana
c. Ujuzi
d. Kujulikana
11. KAMILISHASENTENSI: Walimu wote wamevaa suti__mwalimu kipande
a. Ijapokuwa
b. Ili
c. Ila
d. lakini
12. Ni methali ipi yenye maana sawa na “yakijaa hupwa”
a. Maji yakimwagika hayazoleki
b. Mpanda ngazi hushuka
c. Maji ya kifuu bahari kwa chungu
d. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno
13. Ni sentensi ipi ionyeshayo kivumishi kimilikishi
a. Gari hili jipya
b. Moto mtiifu hupendeza
c. Nyumbani kwao ni kizuri
d. Alifurahi bali hakucheza
14.Tumia viunganishi:____walimu walimshauri ajitahidi, yeye alipuuza___yake aliingia anasa na yake alifeli.
a. ingwa ,hatima, badala
b.isipokuwa,badala,hatima
c .ijapokuwa , badala,hatima
d.ingawa, kabla , hatima
15.ipi si sehemu ya mwili
a.msamba
b.kiko
c.kwapa
d. sura
kiswahili revision papers