2.5. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 3:17 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Bainisha matumizi ya maneno yaliyopigwa mstari katika sentensi.
Nswi huyu ni wangu. Yule pale ni wako
a. kimilikishi. kiwakilishi
b. kiwakilishi, kivumishi
c. kivumishi, kielezi
d. kiashiria, kielezi
2. Kipande cha mbao cha kufungia mguu au mkono uliovunjika ni______
a. machela
b. bendeji
c. kikindiko
d. kitala
3. Chagua orodha yenye vivumishi tasa______
a. mwenye, yeyote, wote, nyingine
b. murua, mahiri, kamili, stadi
c. mrefu, hodari, mbaya, wane
d. vipi, wangapi, lipi, kipi
4. Nomino “kataa” katika kauli ya kutendeshwa ni
a. katazwa
b. katisha
c. katizwa
d. katishwa
5. Ni orodha ipi isiyolingana na me ngine
a. pete, kishaufu, bangili, herini
b. ngombo, ngiri, kondoo, kuku
c. parafujo, timanzi, utepe, randa
d. tai, njiwa, kanga, korongo
6. Wingi wa,”nyani amerauka tawini” ni
a. Nyani wamerauka tawini
b. Nyani wamerauka matawini
c. Manyani wamerauka matawini
d. Manyani wamerauka tawini
7. Kanusha sentensi ifuatayo Nimuonapo ndipo nifurahipo
a. nimuonapo sifurahipo
b. Siomuonapo sifurahipo
c. Nimuonapo sifurahipo
d. Nisipomuona sifurahipo
8. ________ chai hiyo kutoka jikoni kasha _____viazi
a. Injika, ambua
b. Menya, uchote
c. Epua, umenye
d. Injika, uepue
9. Ni sentensi gani rahisi kimantiki
a. niliyatema masuo, nikajisutukua, nikapiga mswaki.
b. nilijisutukua, nikatema masuo, nikapiga mswaki
c. nilipiga mswaki, nikatema masuo, nikajisukutua
d. nilipiga mswaki, nikajiskutua, nikatema masuo.
10. Ali alicheza vizuri ingawa alikuwa mgonjwa. Neno linaloweza kutumiwa badala ya ingawa ni_______
a. mighairi
b. ijapo
c. lau
d. ijapokuwapo
11. Mamkwe na Bamkwe ni wazazi wa_______ wangu
a. mke
b. mume
c. mjomba
d. watoto
12. Ni sentensi ipi isiyoonyesha maana ya neno mori.
a. sehemu ya kuoshea vyombo
b. Mafuta kwenye kifua cha mnyama
c. Hasira kali
d. Ng’ombejike ambaye hajazaa
13. Athari ya hali ya hewa inayofanya ardhi kavu ionekane kama ina maji wakati kuna juakali ni
a. ukame
b. kiangazi
c. mazingazi
d. mazigazi
14. Mkufu huvaliwa shingoni na pete_______
a. mwilini
b. kiwikoni
c. chandani
d. mkononi
15. Chagua kikundi cha wadudu
a. Parare, senene, nyungunyungu, fukufuku, sodomti.
b. Buibui, chale, dumuzi, shwanda, mnandi.
c. Barakoa, nyengere, sungusungu, usumbi, ugomvi.
d. Nyingu, mchwa, nondo, kereng’ende,mburukenge.

kiswahili revision papers