2.6. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 10:41 PM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Tambua nomino baki.
a. Chusere
b. Mwanambee
c. Mziwanda
d. kifungumimba
2. Ni kiunganifu “A” kipi ambacho hakifai katika ngeli ya PAKUMU?
a. la
b. kwa
c. pa
d. mwa
3. mtu aliyepinda vidole vya miguu au vya mikono huitwa______
a. kiduva
b. kibwiko
c. zezeta
d. kithembe
4. umbo la msonge aidha huitwa?
a. Kishada
b. Mche
c. Ngoe
d. pia
5. uovu, uhodari, upendo ni nomino?
a. Dhahania
b. Mahususi
c. Mguso
d. fungamano
6. wanafunzi wote shuleni walipasi vizuri. Kivumishi ni?
a. Vizuri
b. Wanafunzi
c. Walipasi
d. wote
7. kinyume cha shimali ni____
a. yamini
b. matlahi
c. mitlahi
d. kusini
8. kazi za kulazimisha huitwa?
a. Kazi ya koto
b. Kazi ya gunda
c. Kazi ya uluwa
d. Kazi ya ujuma
9. Mahali ambapo akina mama wajawazito hujifungulia huitwa______
a. Ufuoni
b. Kungani
c. Pambajio
d. maliwatoni
10. msimbo alishtakiwa kwa kosa la kula njama ya kupindua serikali. Hilo ni kosa la_____
a. jinai
b. daawa
c. uahini
d. kukata rufaa
11. siku tano kabla ya leo ni____
a. juzi
b. juzijuzi
c. kitondo
d. kitojo
12. pesa zinazotolewa na serikali kwa idara mbalimbali kujiendeleza ni_____
a. mtaji
b. uwekezaji
c. ruzuku
d. utandawazi
13. mseto wa maharagwe na mahindi huitwa ____
a. githeri
b. pure
c. maharagwe
d. mchanganyiko
14. chanja nambari shufwa zote
a. 24
b. 16
c. 30
d. 18
15. Chanja nambari watiri zote
a. 26
b. 30
c. 24
d. 40

kiswahili revision papers