2.7. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 27, 2015, 11:00 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Ni kundi lipi lenye viunganisha pekee?
a. safi,hodari,murua,halali
b. mbali,kando,baidi,karibu
c. hizi,hiki,hicho,Yule
d. ila,ingawa,lakini,licha
2. ni sentensi lipi iliyoakifishwa sawa
a. Aka,yohana hakukuaga!Maajabu haya!
b. Aka! yohana hakukuaga!maajbu haya!
c. Aka!yohana kukuaga?maajabu haya!
d. Aka! yohana hakukuaga? maajabu haya?
3. Nomino ‘’jitu’’iko katika ngeli gani?
a. A-wa
b. I-ZI
c. U-YA
d. LI-YA
4. chagua methali inayoafikana na maelezo haya .watu wengine wanapozozana nakugombana,kunao wanafurahia hali hiyo
A. vita vya panzi furaha ya kunguru
B. majuto ni huha kinyume
C. baada ya dhiki faraja
D. vita havina macho
5. Sentensi ipi si sawa kisarufi
a. Hivi ni vichana ambavyo ni vibaya
b. hizi ni ndizi ambazo zimeiva
c. hizi ni funguo ambazo zimepotea
d. Haya ni mafuta ambazo nayatumia
6. mpango wa michoro ifuatayo ni

Diagram

a. duara,pia,mraba,duaradufu,pembe nne
b. duaradufu,mtatili,pia,duara,mraba
c. pia,duara,pembe nne,duaradufu,mraba
d. pembe nne,pia,duara,mraba,duaradufu
7. vazi ambalo ni suruali imeshonwa pamoja na sharti na hutumiwa wakati wa kufanya kazi huitwa?
a. surupwenye
b. suti
c. kanchiri
d. gauni
8. mwalimu wa darasa la nane aliuliza maana ya neno
mwamu
  i) patero alisema ni mtu mrefu sana
(ii) kimongo alisema ni kakake mumeo
(iii) didi alisema ni kakake mkeo
(iv) somo aliasema ni mototo wa dadako
ni nani kati ya wanafunzi hawa aliyetoa jibu sahihi
a. didi na petero
b. somo
c. didi
d. kimongo
9. maneno yafuatayo ni visawe ila
a. madukan
b. gulio
c. chete
d. soko
10.Andika kwa usemi wa taarifa
‘’Mwanawe ni kiume ,“ Akasema
a. mwana wake ni kiume
b. mwanangu ni wa kiume
c. Alisema kuwa mwana wa mtu huyo ni kiume
d. mwana si kiume
11. Andika kwa wingi
“Mtangulizi mwema huacha msingi imara”
a. watangulizi wema huacha msingi imara
b. mtangulizi mwema haacha msingi imara
c. watangulizi wema haawachi msingi imara
d. watangulizi wema huacha msingi imara
12. Ni nahau ipi iliyo na maana ya kumsifu mtu sana?
a. kumpigia ukope
b. kumpigia debe
c. kumpigia ngoma
d. kumpigia gitaa
13. chagua kikundi cha vimelea
a. kiroboto,kunguni,chawa,funza
b. kitungule,kimatu,buu,shibli
c. kiokozi,karo, ushuru,nauli
d. funza,buibui,nzi,mbu
14. kanusha sentensi ifutayo
mtoto hulia kila asubuhi
a. mtoto hakulia kila asubuhi
b. mtoto hajalia kila asubuhi
c. mtoto hatalia kila asubuhi
d. mtoto hali kila asubuhi
15.Teua kivumishi cha wasaa katika sentensi hii
mwanagenzi yule alijihimu macheo kudurusu mabuku yake
a. macheo
b. mabuku
c. alijihimu
d. mwanagenzi

kiswahili revision papers