2.9. Fasihi Kitengo cha Pili Sehemu ya Tisa - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 29, 2015, 8:03 AM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Tegua kitendawili:Akitoka harudi
a. Jua
b. Mwizi
c. Jani
d. umaskini
2. Ukubwa wa sentensi:mguu wa ng’ombe umepona
a. Guu la ng’ombe limepona
b. Guu la gombe limepona
c. Kiguu cha kigombe kimepona
d. Guu la gombe umepona
3. Chagua kundi lenye mcheka,iga ,oga,soma
a. Ila,isipokuwa,laity,yamkini
b. Tochi,shina,kalamu,faida
c. maneno ambayo ni vivumishi
d. sita,zuri,kali,mpya
4. Waja wote walifika mapema _______ hawakutaka kuchelewa
a. Ili
b. Kwa vile
c. Lakini
d. Kwa kuwa
5. Nomino shida inapatikana katika ngeli gani?
a. LI-YA
b. I-ZI
c. U-I
d. U-ZI
6. Kutokana na nomino malezitunaweza unda kitenzi kipi?
a. Ulezi
b. Mlezi
c. Lewa
d. Lelewa
7. Chagua kundi la magonjwa pekee
a. Kifanduro,malale,pumu,muhina
b. Kisukari,kifua kikuu,kiharusi,mwangwi
c. Upele,kifua kikuu,kiharusi,ukiwa
d. Tetekuwanga,ukosandisha,malaria,tete
8. Ni sentensi ipi sahihi?
a. Nisingekula nisingeshiba
b. Tungeliona gari tungaliondoka
c. Wangezozana wasingeliachiliwa
d. Ungelinunua tunda ungenigawia
9. Ni kipi kisawe cha takia?
a. Foronya
b. Taka
c. Mto
d. kiti
10. huko nje kulikuwa____
a. peupe pepepe
b. kweupe kwekwe
c. nyeupe pepepe
d. kweupe pepepe
11. juma na ali wana umri sawa.kwa hivyo___
a. wanaafikiana
b. wanafanana
c. wanalingana
d. wanatoshana
12. iwapo likizo itaanza siku nne baada ya jana je,itaanza lini?
a. Mtondo
b. Mtondogoo
c. Kesho kutwa
d. kitojo
13. jingo la kufanyia utafiti wa kisayansi huitwa
a. maabara
b. makavazi
c. handaki
d. maabadi
14. Chagua jibu sahihi
ubao huu utumika katika ___________ picha
a. kuandika
b. kuangika
c. kikunga
d. kuunga
15. Tita ni kwa kuni ______ ni kwa vibarua
a. robota
b. bunda
c. kikosi
d. genge

kiswahili revision papers