3.0. Fasihi Kitengo cha Tatu Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 11:06 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Aug 3, 2015, 9:17 PM ]

Kutoka swali la 1 mpaka 15, chagua jibu lililo sahihi


1. Chagua kundi lenye viunganishi vya kuonyesha kasoro au kinyume cha matarajio
A. Licha ya, isitoshe, fauka ya
B. Isipokuwa, lakini, minghairi
C. Miongoni mwa, lengo la, mithili ya
D. Angalau, kabla ya, madhumuni
2. Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa.
‘’siondoki hapa mpaka nimuone motto wangu’’,mama alisema
A. Mama alisema asingeondoka hapo mpaka amuone mtoto wangu.
B. Mama alisema hataondoka hapa mpaka atakapomwona mtoto wake
C. Mama alisema asingeondoka pale mpaka ambapo angemwona mtoto wake
D. Mama alisema asingeondoka hapo mpakaatakomwona mwana wake.
3. Ni sentensi gani iliyo katika hali ya kutendewa
A. nitakununulia daftari jingine zuri
B. paka amemkimbiza panya mkubwa
C. maneno yako yamesikika vizuri
D. kibarua alipelekewa chakula shambani
4. Chagua sentensi iliyokatika nafsi ya tatu kwa wingi
A. Sisi sote tumeenda ukumbini
B. Wanafunzi wale walipita mtihani
C. Mwanafunzi Yule amepita mtihani
D. Nyinyi mmepita mtihani vizuri
5. Ni sentensi gani ambayo ina kielezi takriri
A. Amenipiga bure bilashi
B. Penseli imeanguka ikavunjika kacha
C. Kamene ni chiriku
D. Tunasaidiana kama kinu na mchi
6. Kinyume cha sentensi ifuatayo ni kipi
Aghalabu uhuru hupendwa na vijana
A. Kwa nadra utumwa huchukiwa na wazee
B. Mara nyingi utumwa huchukiwa na wazee
C. Kwa nadra uhuru hupendwa na wazee
D. Aghalabu utumwa huchukiwa na vijana
7. Andika wingi wa sentensi ifuatayo:
Ufa uliyo kwenye sakafu utarekebishwa kwa waya
A. Nyufa zilizo kwenye masakafu zitarekebishwa kwa nyaya
B. Nyufa zilio kwenye sakafu zitarekebishwa kwa nyaya
C. Nyufa zilizo kwenye sakafu zitarekebishwa kwa nyaya
D. Nyufa zilizoko kwenye sakafu zitarekebishwa na waya
8. Andika wingi wa udogo wa sentesi ifuatayo
Nyumba hiyo ilijengwa na mtu mwenye tajiriba
A. Kijumba hicho kilijengwa na kijitu chenye tajiriba
B. Majumba hayo yalijengwa na majitu yenye tajiriba
C. Vijumba hivyo vilijengwa na vijitu vyenye tajiriba
D. Chumba hicho kilijengwa na kijitu chenye
9. Methali ipi yenye maana sawa na:
Meno ya mbwa hayaumani
A. Mbwa hafi maji akiona ufuo
B. Ndugu wawili waligombana chukua jembe ukalime
C. Jino la tembo si dawa ya pengo
D. Jino halinyimwi mcheshi
10. Bainisha matumizi ya maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi
Mwanafunzi huyu ni wangu, Yule pale ni wako
A. Kivumishi, kiwakilishi
B. Kielezi, kiwakilishi
C. Kivumishi, kielezi
D. Kiwakilishi, kivumishi
11. Ni sentesi gani ambayo imetumia wakati tegemezi kwa usahihi
A. Tulipofika alikuwa akiongea na mwalimu
B. Kama hangeenda hangepewa nafsi ya kazi hiyo
C. Ametuita mkutanoni ili tuboreshe mazingira
D. Maria angaliongoza kama angalifanya mazoezi zaidi
12 .I chagua sentensi yenye KI ya kivumishi cha kufananisha
A. Wachezaji ngoma wamevaa mavazi ya kiafrika
B. Nikiondoka mapema nitampata
C. Kikombe kimewekwa chai
D. Wanaongea kisirisiri
13 Jina waitanalo wazazi wa mume na wazazi wa kike ni:
A.Mwanyumba
B. Mcheja
C. Maharimu
D. kivyere
14. Ni neon lipi lisiloonyesha rasilimali ya kiasili
A. Viwanda
B. Kichaka
C. Bahari
D. Maji
15. Hatua ya mwisho katika uandkaji wa kumbukumbu ni ipi?
A. Anwani
B. Ajenda
C. Thibitisho
D. Waliohudhuria

kiswahili revision papers