1.2. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 8:55 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 7. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Malkia alivua __1__ wake kichwani akamtazama kitwana huyo kwa hasira asijue la kufanya. Hakuweza kuamini __2__. “si huyu aliyekuwa mtumishi wangu mwaminifu?” __3__ kimoyomoyo. “kwa nini akanifanyia hivyo licha ya__4__niliyomtendea? Alikumbuka alivyomwokota kijana huyo akichumia chungu mekoni hana hali ala mali, akifanya vibarua __5__, __6__mpaka akaonekana nadhifu; akampa kazi, tegemeo na usalama. “Leo hii anathubutu __7__kiasi hiki? Ama Kweli ivushayo ni mbovu.”
1. A. Ukanda     B. utaji      C. utepe     D. ukosi
2. A. aliyoyasikia      B. aliyasikia     C. aliyeyasikia     D. aliosikia
3. A. akajisema      B. akamsema     C. akamsemea      D. akajisemea
4. A. mingi B. wengi C. mengi D. nyingi
5. A. vidogovidogo B. ndogo C. kidogokidogo D. dogo
6. A. akamfuza B. akamtunza C. akamtunzia D. akamtuzia
7. A. kumdhulumu B. kudhulumu C. kuwadhulumu D. kunidhulumu

1.2. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Pili - Majibu [you need to sign in first and to sign in, you must be a member]


1.1. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Kwanza - Maswali

Nyuma

Kwa majibu yaliyo na dosari, tuma malalamishi kwa sales@manyamfranchise.com
kiswahili revision papers