1.4. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 5:43 AM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Katika __1__ ya malezi ya watoto, wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto __2__ kuhusu uwekaji akiba na utunzaji wa mali yao na __3__ watu wengine.
Kadhalika, wazazi wana jukumu __4__ kuwafahamisha watoto kwamba maisha yana changamoto __5__ hivi kwamba bidii na __6__ ni nguzo muhimu katika maisha. Ka hivyo, wazazi kamwe hawapaswi kuwadekeza watoto nyumbani katika mazingira ya nyumbani, watoto amepaswa kupatiwa majukumu madogo madogo __7__ vile kujifulia nguo zao kwa mfano nguo za ndani, kujitandikia vitanda vyao na kunadhifisha vyumba vyao vya kulala.
__8__ watoto wanapokuwa hawaendi shule, anapaswa kupewa majukumu ya kuosha vyombo na kupanguza meza __9__ ya kula. Ikiwezekana watoto wanapaswa kufundishwa jinsi ya kupika hasa kwa kutumia meko mbalimbali kama vile stovu, jiko la makaa au hata gesi.
Kufanya hivi __10__ msingi bora wa kujisimamia na kujitegemea punde wanapokuwa watu azima na kuishi kivyao.
Mzazi anayemkataza mtoto __11__ kufanya kazi za kimsingi ni mzazi aliyeshindwa na jukumu lake.

1. A. maisha    B. shughuli    C. namna    D. kawaida
2. A. yao    B. zao    C. wao    D. wako
3. A. ya    B. wa    C. yenya    D. za
4. A. la    B. ya    C. wa    D. na
5. A. mingi    B. ingine    C. nyingi    D. kidogo
6. A. kuwategemea    B. kumtegemea    C. asitegemee    D. kujitegemea
7. A. na    B. kama    C. ingawa    D. hasa
8. A. maana    B. maadamu    C. aidha    D. minghairi
9. A. kabla    B. baada    C. mbele ya    D. baadaye
10. A. inawasaidia    B. inawawezesha    C. kunawapangia    D. kunawawekea
11. A. wake    B. yake    C. wao    D. wangu

Watoto wanapaswa pia kufahamishwa kwamba mali yoyote nyumbani hupatikana __12__ njia ngumu na wala haipaswi kutumiwa vibaya. Watoto __13__ katika familia tajiri wanaweza kupotoka hasa kwa kuchukulia kwamba mali ya wazazi wao ni yao.
Mzazi __14__ anapaswa kueleza wazi kwamba mali aliyo nayo ni yake. Hivyo basi, tangu utotoni, wazazi wanapaswa kuweka __15__ za kuwaongoza watoto wao kuhusiana na masuala haya.

12. A. katika    B. bila    C. kwa    D. kwenye
13. A. walewao    B. wanaolewa    C. wanaotunzwa    D. wanaolewa
14. A. mtajiri    B. mkwasi    C. mbaya    D. maskini
15. A. sheria    B. mwiko    C. desturi    D. mila   
kiswahili revision papers