1.6. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:02 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Giza katika kiambo changu___1__.  Wezi   walianza kukimbia lakinihawakujua pa kutokea kwani nyyumba ilizungukwa na__2__. Majirani nao walijua fika kuwa__3__. Walijitokeza wakiwa na silaha mikononi. Kelele zao zilinifanya kuwakisha__4__.Mama we! Majambazi walikuwa waking’ang’ania kuyanusuru maisha yao.   Punde si punde walibebwa hangahanga wakipokea makonde na mateke.  Walipigwa __5__ huruma. Damu iliwatiririka __6__. Waliomba msamaha __7__ hakuna aliyekuwa na nia ya kuwasamehe. Kichapo kile kilikuwa kama __8__. Walipigwa sana.

1    A. lilitisha                 B. ulitisha            c. ilitisha            D. kilitisha
2    A .ua refu      B.ua ndefu     C.ua mrefu      D.ua lirefu
3    A.penye wazee hapaharibiki neno     C.pwagu hupata pwaguzi      B.penye moshi panafichamoto     D.mwenye kovu usidhani kapoa
5    A.kwa    B.na      C.bila    D.vya
6    A.kama maji mliman    C.kama machozi yanayoengaenga    B.kama maji ya bilula    D.kama mwangwi porini
7    A.kwa hivyo    B.kwa vile    C.lakini    D.kwa kuwa
8    A.kazi ya sulubu    B.kazi ya hiari     C.kazi ya kijungu jiko     D.kazi ya goya

Haijalishi kama mahuluki ameyasoma__9__.  Haijalishi kama amefikia kiwango au__10__ shahada zipi? Iwapo hana adabu, heshima, nidham na uajibikaji, elimu yake haijakamilika. Elimu hiyo yote si chochote si lolote.Elimu yake itakuwa kama pambo wala si lebasi.Pambo haliwezi__ 11__ na mtu.Hiyo ni kazi ya nguo.Ni __12__ kuwaona baadhi ya insi wakichachowiza kuwa wameelimika __13__ wanazo fusika.Heshima kwao ni__14__. Adabu kwao ni neno __15__.

9      A. matopa ya vitabu       C.makundi ya vitabu  B.vifurushi vya vitabu        D.marundo ya vitabu
10    A.anayo       B.analo       C.anazo       D.wanayo
11    A.kukomesha        B.kusitiri        C.kuangamiza     D.kuhiliki
12    A.simanzi na majonzi   B.balaa  na  belua   C.tunu na tamasha        D.fedheha  na izara
13    A.kumbe         B.ilhali        C.ingawa        D.lo!
14    A.mwiko       B.kawaida    C.desturi       D.kitiba
15    A.mgeni        B.ngeni        C.ligeni        D.geni

kiswahili revision papers