1.7. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:03 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Giza katika kiambo changu __1__. Wezi walianza kukimbia lakini hawakujua pa kutokea kwani nyumba ilizungukwa na __2__. Majirani nao walifahamu fika kuwa __3__. Walijitokeza wakiwa na silaha mikononi. Kelele zao zilinifanya kuwakisha__4__. Mama we! Majambazi walikuwa waking’ang’ania kuyanusuru maisha yao. Punde si punde walibebwa hangahangawakipokea makonde na mateke. Walipigwa __5__ huruma. Damu iliwatiririka __6__. Waliomba msamaha __7__ hakuna aliyekuwa na niya ya kuwasamehe. Kichapo kile kilikuwa kama __8__. Walipigwa sana.
1.  A. Lilitisha     B. ulitisha        c. ilitisha          D.kilitisha
2.  A. ua refu      B. ua ndefu     c. ua mrefu     D. ua lirefu
3.  A. penye wazee hapaharibiki jambo           B. penye moshi panafisha  moto    C.pwanguhupata pwaguzi       D. mwenye kovu usidhani kapoa
4.  A. mataa yote   B. mataa zote    C. taa yote    D. taa zote
5.  A. kwa                B. na                     C. bila           D. vya
6.  A. kama maji mlimani      B. kama maji bilula    C. kama machozi yanayoengaenga       
D. kama mwangwi porini
7.  A. kwa hivyo      B. kwa vile          C. lakini           D. kwa kuwa
8.  A. kazi ya sulubu  B. kazi ya hiari   C. kazi ya kijungu jiko   D. kazi goya   

Haijalishi iwapo mahuluki ameyasoma __9__. Haijalishi amefikia kiwango kipi au __10__ shahada zipi? Iwapo hana adabu , hershima, nidhamu na uwajibikaji, elimu yake haijakamilika. Elimu hiyo yote si lolote si chochote. Elimu  yake itakuwa kama pambo wala si lebasi. Pambo haliwezi __11__ mtu. Hiyo ni kazi ya nguo. Ni __12__ kuwaona baadhi ya insi wakichachizwa kuwa wameelimika __13__ wanazo  fuska. Heshima kwao ni __14__. Adabu kwao ni neon __15__.


9.  A. matopa ya vitabu   B. vifurisha vya vitabu   c. maku ndi ya vitabu    D. marundo ya vitabu

10. A. anayo    B. analo   C. anazo  D. wanayo
11. A. kukomeasha    B. kusitiri    c. kuangamiza    D. kuhiliki
12. A. simanzi na majonzi  B. balaa na belua  c. tunu na tamasha  D. fedheha na izara
13. A. kumbe    B. ilhali    C. ingawa     D. lo!
14. A. mwiko     B. kawaida   C. desturi    D. kitiba
15. A. mgeni     B. ngeni         C. ligeni      D. geni
kiswahili revision papers