1.8. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Nane - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:04 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Katika dini __1__ ,wanawake  __2__ na makosa  ya  __3__ walikuwa wakipigwa huku wenzao wanaume  __4__ .Ukisoma  __5__ utasoma kisa cha mwanamke  __6__ baada ya yesu  __ 7__  __8__ kwamba  ni Yule ambaye hana __9__ anayestahili  kumrushia __10__.
Hata wewe sasa __11__ kosa la magari __12__ abiria kupita __13__ huchangiwa  na abiria  __14__  gari licha ya kuona __15__ .Bodi ya leseni za uchukuzi (TLB)haicheli na wewe tena . Mwenyekiti  wake , Wilfred  amesema utakuwa ukishtakiwa pamoja na  madereva .

1.       A. Mingi         B. Kwingi           C. nyingi         D. wengi
2. A. hawangepatikana   B. waliopatikana    C. wanaatukana  D. wangekuweko
3.       A. kuimba        B.kaskazini          C.kusini          D.kuzini
4. A. wakiponyoka     B.wakiponyokeshwa    C.wakisini   D.wakitamani pia
5.       A.kurani         B. bibilia               C. bibria         D.biblia
6. A. aliyejeruhi    B. aliyejikwaa     C .aliyenusuru   D. aliyenusurika
7.       A. kuwakumbusha          B. kuwaonya      C.kuwaarifu        D.kuarifu
8. A. waliomuhukumu   B. waliojihukumu    C.wangepahukumu   D.hawahukumu
9.       A.lengo         B.hatia             C.jukumu            D.wazo
10.   A. machozi  B.mate    C. vumbi   D. jiwe
11.   A. kujikwaa         B .kuanguka       C. kuponyoka    D.kutuleza
12.  A. kubeba   B.kuacha    C.kuiba    D. kupokora
13.   A. kiazi                  B. kiasi                  C. katikati            D. moja
14.  A.wanaoabudu   B. wanaosubiri    C. wanao   D. wanaoabiri
15.   A. limejaa            B. halina mtu                      C. umejaa                            D.liko
kiswahili revision papers