1.9. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Tisa - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:05 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Siku moja __1__matembezi__2__,__3__kobole aliskia kelele,’wachomeni__4__.  Hakuna kuwahurumia ‘Mama akichungulia kumbe ni mabarobaro wawili waliofungwa kamba.__5__ __6__alikuwa Kobole akiwa anachuruzika damu __7__uso__8__.Mama alianguka na kupotewa na fahamu. Walimpora mwanamke mtalii mkoba wake watu walieleza. Mwalimu wa Kobole alikuwepo hapo__9__,’msiba wa kujitakia hauna __10__mwalimu mkuu halikadhalika alikuwepo na akasema,Asiyefunzwa na mamaye hufunawa na ulimwengu.

1.     A.kwa      B.kuwa     C. katika    D. kwenye
2. A. yake     B.chake     C. wake     D. mwake
3.     A. mamawe     B.mamao     C. mamayo     D.mamake
4. A. wao     B. hao     C. chao     D.mwao
5.     A. moja     B. mmoja     C. kimoja     D. mamoja
6. A. hayo     B.yao     C. wao     D.mwao
7.     A. chururu     B. chiriri     C. tiriri     D. rururu
8. A. nzima     B. zima     C. msimu     D. mzima
9.     A. alisema     B. akasema     C. anasema     D. atasema
10. A. mlio   B. machozi     C. kilio    D. huruma

Tulifika dukani __11__lugha –mama. Mimib nilikuwa__12__kiswahili __13__cha haja licha Ya.”hujambo sijambo” Martin aliingia __14__ kununua bidhaa__15__.

11.   A. tukiongea     B. tunasema     C. tukisema     D. wakingea
12. A. ninasema  B. sijaona  C. sijaelewa  D. sijasema
13.   A. lolote     B.chochote     C . wowote     D.kokote
14. A.nyumbani  B. duka  C. zizini  D. dukani
15.   A.  tulizotumwa     B.tuliyotumwa     C.walizotumwa     D. waliyotumwa
kiswahili revision papers