1.0 Kifungu cha Kwanza Sehemu Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:55 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 8:49 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 8. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Giza katika kiambo changu __1__. Wezi walianza kukimbia lakini hawakujua lakini hawakujua pa kutokea kwani nyumba ilizungukwa na ___2___. Majirani nao walifahamu fika kuwa __3__. Walijitokeza wakiwa na silaha mikononi. Kelele zao zilinifanya kuwakisha __4__. Mama we! Majambazi walikuwa waking’ang’ania kuyanusuru maisha yao. Punde si punde walibebwa hangahanga wakipokea makonde na mateke. Walipigwa __5__ huruma. Damu iliwatiririka __6__. Waliomba msamaha __7__ hakuna aliyekuwa na nia ya kuwasamehe. Kichapo kile kilikuwa kama __8__. Walipigwa sana.
1. A. lilitisha          B. ulitisha         C. ilitisha          D. kilitisha
2. A. ua refu         B. ua ndefu      C. ua mrefu     D. ua lirefu
3. A. Penye wazee hapaharibiki nene     B. Penye moshi panaficha moto C. Pwagu hupata pwaguzi  D. Mwenye kovu usidhani kapoa
4. A. Mataa yote     B. mataa zote     C. taa yote     D. taa zote
5. A. kwa         B. na         C. bila         D. vya
6. A. Kama maji milimani   B. Kama maji ya bilula   C. Kama machozi yanayoengaenga    D. Kama mwangwi porini
7. A. Kwa hivyo         B. Kwa vile         C. Lakini         D. Kwa kuwa
8. A. Kazi ya sulubu     B. Kazi ya hiari     D. Kazi goya    C. Kazi ya kijungu jiko
kiswahili topical questions