1.1 Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:39 AM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 7. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Haijalishi iwapo mahuluki ameyasoma__1__. Haijalishi amefikia kiwango kipi au __2__ shahada zipi? Iwapo hana adabu, heshima, nidhamu na uajibikaji, elimu yake haijakamilika. Elimu hiyo yote si lolote si chochote. Elimu yake itakuwa kama pambo wala si lebasi. Pambo haliwezi __3__mtu. Hiyo ni kazi ya nguo. Ni __4__ kuwaona baadhi ya insi wakichachowiza kuwa wameelimika__5__ wanazo fuska. Heshima kwao ni __6__. Adabu kwao ni neno __7__.

1. A. matopa ya vitabu     B. vifurushi vya vitabu      C. makundi ya vitabu     D. marundo ya vitabu
2. A. anayo      B. analo     C. anazo     D. wanayo
3. A. kukomesha      B. kusitiri     C. kuangamiza      D. kuhiliki
4. A. simanzi na majonzi B. Balaa na belua C. tunu na tamasha D. fedheha na izara
5. A. kumbe B. ilhali C. ingawa D. lo!
6. A. mwiko B. kawaida C. desturi D. kitiba
7. A. mgeni B. ngeni C. ligeni D. geni

1.1. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Kwanza - Majibu [you need to sign in first and to sign in, you must be a member]

1.2. Kifungu cha Kwanza Sehemu ya Pili - Maswali

1.0. Kifungu cha Kwanza Sehemu Nunge - Maswali


Nyuma

kiswahili revision papers