2.0. Kifungu cha Pili Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:06 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Mahakama ilikusanyika tena__1__za alasiri. Zablon alitolewa kutoka mojawapo ya __2__ za chini __3__ mahakama na kusindikizwa __4__ chini __5__ ulinzi __6__.Alitolewa __7__ na kuachwa amesimama pale akaitwa __8__.Ilikuwa dhahiri __9__ kwamba mwazo yake yalikuwa __10__.

1. A. zaa     B. shaa     C. saa     D. jaa
2. A. seli     B. seri     C. sheli     D. sheri
3. A. na     B. wa     C. kwa     D. mwa
4. A. mumbani     B. jukwani     C. kizimbani     D. ukingoni
5  A. wa     B. ya     C. za     D. na
6. A. kali B. mkali C. mkari D. kari
7. A. mbingu     B. pinga     C. pingu     D. bingu
8. A. ametumwaa     B. ameduwaa     C. amenduwaa     D. amedwaa
9. A. shahiri     B. sahiri     C. shahili     D. shairi
10. A. bali     B. mbali     C. mbari     D. bari

Usalama barabarani umeimarika n__11__serkali __12__ nguvu sheria zote __13__ kuwa kila gari la __14__ liwe na kidhabiti mwendo mikanda ya usalama na __15__ abiria wengi kuliko inavyoruhusiwa na leseni yake.

11. A. mpaka     B. tangu     C. hadi        D. kwa
12. A. ilipotia     B.zilipotia     C.inapopota     D. ilitia
13. A. ya     B. zake     C. kwa     D. za
14. A. uma     B. watu     C. umma     D. dala
15. A. lisibebe     B. isebebe     C. ubebe     D. zisibebe

kiswahili revision papers