2.1. Kifungu cha Pili Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:07 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Nyani __1__alikuwa akiona njaa. Akatamani sana apate kitu__2__ ili ashibe. Alianza kutafuta __3__ za kupata mlo. Mara alitokeza __4__ shamba__5__ mahindi __6__ sana. Alianza __7__ pupa na papara kama fisi __8__ kupindukia. Alihakikisha __9__ amezunguka kote shambani__10__ huku akiendelea kubugia, matunda, maharagwe, viazi na muhogo. Mwenye shamba __11__ alimkuta nyani amelala__12__ huku__13__ kama paka. Alianza kumpiga__14__ hasira. Nyani alilia akiwa na huzuni__15__ lakini hakuna aliyemwonea huruma hata mmoja.

1. A. moja      B. mmoja     C. kimoja      D. wamoja
2. A. akule      B. kukula     C. ale     D. wakule
3. A. upande     B. wakati     C. mbinu     D. njia
4. A. kwa      B. ndani     C. katika      D. enye
5. A. na      B. la     C. ya     D. wa
6. A. nyingi     B. mingi      C. mengi      D. kingi
7. A. kula na     B. kukula kwa      C. kula kwa      D. kukula na
8. A. mlafi      B. mlaji     C. mkulaji     D. mlefi
9. A. kwa     B. kuwa     C. kua     D. kukuwa
10. A. lote      B. pale     C. lile     D. kule
11. A. alifika      B. alikofika     C. alipofika     D. alimofika
12. A. fefefe      B. fofofo     C. ndindindi     D. kekeke
13. A. aking’orota      B. akingumma     C. akikoroma      D. akilalama
14. A. na      B. kwa     C. wa      D. za
15. A. mwingi     B. mingi     C. nyingi      D. mengi

kiswahili revision papers