2.2. Kifungu cha Pili Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:09 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Nidhamu ni utaratibu ____1___ jambo.Ni kuwa na __2_____ katika kutekeleza jukumu _____3____.Mwenye nidhamu hutenda mambo yote kwa ____4____ na . Moyo wake humwonya _____5_____ ya kujihusisha na mambo maovu yanayoweza kumletea ____6____ na kwa wengi vitendo vyake ____7____ kama usiku na mchana .Akiwa ____8____ au akiwa peke yake hujiepusha na matendo ____9____ ambayo ni ufisadi . Wanapoangazia kutenda jambo hujitahidi kwa ___10___ ____11____ wafue dafu. Hawapendi yeyote wala ____12____ yeyote .Mtu mwadilifu hufanikiwa katika jambo lolote analotenda na ____13__ kama mgomba .Mwenye nidhamu _____14_____ katika jambo lolote ___15___ na atalitenda kwa moyo wa dhati .

1. A. kuendesha     B. kupeleka     C.kuendeshwa      D. kuendeshea
2. A. maoni      B. staha     C.jambo      D.chuki
3. A.lolote     B.yoyote     C.zozote      D. chochote
4. A. kuangalia     B. mwangalifu      C. uangalifu      D.kuangaria
5. A. kinyume     B. dhidi     C. baada     D.muda
6. A.fedha      B. sifa      C.fedheha      D. manufaa
7. A.huwa      B.huhitilafiana      C.husabahiana     D. hulingana
8. A. hadharani     B. hadhirani     C hasarani      D. asarani
9. A. mema      B. chafu     C. mawi     D. mbovu
10. A. hali na mali     B. jino na kucha     C. kufa na kupona     D. kushoto kulia
11. A. kwa sababu     B. ijapokuwa     C. aghalabu     D. almuradi
12. A. kumhudumia      B. kumfaa     C. kumdhulumu      D. kumwauni
13. A. kumea     B. kuchanua      C. kushipuka     D. kunawiri
14. A. hujibika     B. huwajibika     C. hujibiwa     D. huwajibia
15. A. atakaloaminiwa      B. akiaminiwa      C. analoaminiwa      D. anaaminiwa
kiswahili revision papers