2.3. Kifungu cha Pili Sehemu ya Tatu - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 19, 2015, 9:28 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Ni__1__kadhaa__2__ na mwalimu huyo.Alikuwa mwalimu__3__ sana katika lugha ya Kiswahili.__4__ mwalimu huyo alikuwa na__5__moja. Alikuwa na hasiraza__6__. Jambo __7__ tu__8__akasirike vilivyo. Sisi__9__ tulimpendana kumtumia lakini__10__ alipopandwa na__11__ tulikuwa__12__ kwa woga. Katika hali kama hiyo, macho yake ya__13__ yangebadilika rangi na kuwa__14__. Daima dawama sitasahau mwalimu huyo aushini__15__.

1. A. vitu B. mambo C. masaibu D. malalamiko
2. A. tulichofunzwa B. tuliofunzwa C. tuliyofunzwa D. tulizofunzwa
3. A. mstadi B. mhodari C. hatari D. stadi
4. A. ndiposa B. licha C.ingawa D. hata hivyo
5. A. jambo B. ila C. ulaghai D. tatizo
6. A. mvi B. chatu C. mkizi D. samba
7. A. dogo B.ndogo C. kidogo D. lidogo
8. A. lingetuma B.linafanya C. lingesababisha D. likasababishwa
9. A. wote B.nyote C.zote D.sote
10. A.saa B. pindi C.vile D. yeye
11. A. roho B. mori C. pepo D. majonzi
12. A. tukiti a mvija B.tukishika tama C. tukifyata ulimi D. tukicheza ngoma goya
13. A.mbuni B.bisi C. upanga D. kikombe
14. A. mekundu B. nyekundu C. wekundu D.na mekundu
15. A. yangu B. zangu C.wangu D. mwangu
kiswahili revision papers