2.4. Kifungu cha Pili Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 6:12 AM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Tatizo __1__­­­­­­­­­­­­lilionekana kuwa __2__mno mwanzoni. Hakuna __3__ aliyedhani kwamba mambo yangeenda__4__ hatimaye. Utukutu wa kitindamimba wetu__5__ kuwa jambo la kawaida tu__6__. Hatuku fikiria kuwa ungetusababishia__7__ mkubwa kama ule uliotokea na__8__ hasara kubwa. Alikuwa akichezeachezea__9__ cha moto wakati upepo ulipopeperusha__10__ moto hadi paani. Ghafla, moto mkubwa ukatokea. Harakati za __11__moto ule zikaanza. Majirani nao wakawasili kwa wingi ili kutupiga__12__ kupambana na janga__13__ ghafla. __14__ jitihada zetu za kufa kuponea, moto haukuonekana kupungua. Tulitumia chochote kuuzima; maji, mchanga, matawi yamiti na hata vijiti kwani__15__.

1.    A. yenyewe B. mwenyewe C. lenyewe D. enyewe
2.    A. dogo B. lidogo C. ndogo D. mdogo
3.    A. yoyote B. yeyote C. wowote D. popote
4.    A. shwari B. segemnege C. heri D. joshi
5.    A. haukuonekana B. haukuwa C. ulikuwa D. ulionekana
6.    A. hatimaye B. mwishowe C. baadaye D. mwanzoni
7.    A. mkasa B. hasara C. shida D. janga
8.    A. kuzukia B. kuzuka C. kuzuia D. kuzusha
9.    A. kichaka B. jiko C. kijinga D. kijivu
10.   A. mrindimo wa B. nuru ya C. cheche ya D. ndimi za
11.   A. kuuwasha B. kuuchochea C. kuupoza D. kuuzuia
12.   A. jeki B. moyo konde C. hatua D. pambaja
13.   A. hiyo ya B. hayo ya C. hilo la D. hizo za
14.   A. kwa sababu ya B. licha ya C. fauka ya D. kufuatia
15.   A. jitihada haiondoi kudura
B. mtaka yote hukosa yote
C. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
D. fimbo iliyo mkononi ndiyo iuayo nyoka

kiswahili revision papers