2.7. Kifungu cha Pili Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 9:49 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Kwa__1__ watu hawaelewi lugha moja ,wasafiri __2__ kiungo muhimu __3__ mawasiliano kati ya watu wanaosoma lugha mbalimbali.Hata hivyo __4__ ya __5__ katika vyombo__6__ habari ni kubwa zaidi kutokana na sababu kadha wa kadha.Sababu hizi ni __7__ ,vyombo vya habari kama vile redio ,runinga na magazeti huwafikia __8__; pili ,lugha ya vyombo vya habari kama vile redio ,runinga na magazeti hufikiriwa na wengi kuwa __9__ sahihi na sanifu na kwa hivyo ni mfano wa kuigwa.Kwa kweli taaluma nzima ya uanahabari inajishugulisha na kusafiri,kauli __10__,simo n.k kwa maana ya kusahilisha mawasiliano kwa hadhira.__11__ ,baada ya waziri wa fedha kusoma hotuba ndefu ya makadirio ya matumizi ya fedha za serikali katika lugha __12__na iliyokitiwa__13__sajili ya taaluma uchumi ,vyombo vya habari vina wajibika kuitafsiri hotuba hiyo kwa wananchi wa __14__ kwa maneno machache yanayomsaidia kuelewa maana __15__mwenendo na msukumo wa hotuba nzima.
1.      A. kile     B. hivyo      C.vile     D. zile
2.      A.huo  B.huwa C.wakiwa D.mkiwa
3.      A.kwa      B.kua     C.kwamba     D.katika
4.      A.wima B.thima C.dhima D.hima
5.      A.usafiri      B.msafiri     C.safari     D.msafara
6.      A.cha B.vya C.la D.wa
7.      A.mwanzo      B.chanzo      C.mosi     D.pili
8.       A.mengi B.wengi C.vingi D.kingi
9.       A.ndiyo     B.ndilo      C.ndio     D.ndizo
10.     A.waama B.dhana C.hana D.thana
11.     A.mingaeri      B.sembuse     C.mathalani     D.mithalani
12.     A.changamka B.changamani C.changamka D.changa
13.     A.mwa     B.kuwa     C.kwa     D.kwenye
14.     A.kawaida B.kawaita C.kawaita D.kati
15.     A. .      B. ,     C. !     D. ?
kiswahili revision papers