2.9. Kifungu cha Pili Sehemu ya Tisa - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 26, 2015, 3:51 AM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Viongozi wa tume ya kutetea haki za binadamu walishtumu __1__ watu wenye__2__ serikalini wakidai kuwa wanajaribu kuzizimia ___3__za kutetea haki za binadamu. Wanakamati hao pia wa lishtumu serikali kwa kupuuza vita __4__ ufisadi na __5__ kupigwa marufuku. shughuli za tume katika __6__kutetea haki za waja .Walikuwa __7__maswali kwamba wao ni wafisadi sugu na walituma taratibu __8__ kupata bidhaa tumbi nzima.

1. A. ujuzi B. baina ya C. baadhi ya D. miongoni mwa
2. A. ujuzi B. uajibikaji C.uzalendo D. mamlaka
3. A. majukumu B. juhudi zao C. matakwa yao D. mapendekezo
4. A. dhidi ya B.licha ya C.juu ya D. baada ya
5. A. kula njama B. kula rushwa C. kupiga darubini D. maadili ya
6. A. maeneo ya B. harakati ya C. masharti ya D. maadili ya
7. A. watajibu B. wamejibu C. wakijibu D. wakibu
8. A. zinazoeleweka B. zisofaa C. zinazoaminika D. zinazopendeza

Tumeshuhudia __9__kwa magonjwa ja ajabu.Magonjwa hayo __10__watu na __11__bongo za wanasayansi na matabibu katika kutafuta tiba. Magonjwa __12__ tauni,kifua kikuu homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale __13__ maisha ya binadamu hapo zamani. Maradhi haya __14__ maelfu ya watu na __15__uchumi wa nchi.

9. A. kusuka B. kushuka C.kutibiwa D.kuzuka
10. A. yamewahamasisha B. yamewaharakisha C. yamewahangaisha D. yamewadumisha
11. A. kuzishughulisha B.kuzifedhesha C. kuzituliza D. kuzifurahisha
12. A. mbali mbali B. kamavile C. zaidi ya D. ya kuambukiza
13. A yaliyodumisha B. yaliyotisha C. yaliyoimarisha D. yaliyoboresha
14. A. alizuia B. yalibadilisha C. yaliangamiza D. yalihinikiza
15. A. kuendeleza B. kuudhoofisha C. kuupanua D. kuuchochea
kiswahili revision papers