3.0. Kifungu cha Tatu Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Aug 1, 2015, 10:12 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


1. Ni maamkizi yapi yaliyotumiwa kimkosa.
a. Alamsiki _usiku
b. Masalkheri_mchana
c. Sabalkheri_asubuhi
d. Pole_kwa huzuni
2. Kipusa ni msichana mrembo . Maana yake ya pili ni
a) Ghulama mrembo
b) Pembe ya kifaru
c) Aina ya wanyama
d) Samaki wa kike
3. Eleza maana ya methali hii
La kuvunda halina ubani
a. Cha kuvunda kinanuka
b. C ha kuvunda huleta mazuri
c. Cha kuoza hakinuki
d. Cha kuharibika hakifichiki
4. Chagua udogo wa sentensi ifuatayo
Nyoka aliyemwuma ngombe ni huyu
a. Kijoka kilicholiuma gombe ni hiki
b. Kijoka kilichokiuma kigombe ni hiki
c. Joka lililoliuma gombe ni hili
d. Joka kilichokiuma kigombe ni hiki
5. Mpishi alipara samaki .Aliondoa _____
a. Ukoko
b. Maganda
c. Magamba
d. Matumbo
6. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri kati ya hizi
a. Salaala, mbuzi amekula mtoto,mama alimaka.
b. Salaala? mbuzi amekula mtoto! Mama alimaka.
c. “Salaala!Mbuzi amekula mtoto!” Mama alimaka.
d. “Salaala !” Mbuzi amekula mtoto?” mama alimaka.
7. Ambatanisha mambo haya na majina yao
a. Mstahili,mstari,sambamba,zigizagi
b. Mshazari,mduara,duara dufu ,zigizagi
c. Duara,mistarisambamba,mduara ,mshazari
d. Mviringo,mikuki ,duara,mistari nyoka
8. Chagua sentensi iliyo sahihi kisarufi
a. Msichana ambaye alifaulu amesidiwa
b. Wakati ambao umepita imerudishiwa
c. Msichana aliyefaulu ametuzwa zawadi
d. Msichana aliyefaulu ametunzwa zawadi
9. Ni sentensi ipi iliyo na ‘ki’ ya wakati?
a. Kati kinanifinya
b. Alikuwa akicheza uwanjani
c. Kigugumizi amepata zawadi
d. Kile kitu ni kibaya
10. Mwalimu tatu aliingia darasani na muwa mrefu alipowagawia wanafunzi wake ashara ,kila mwanafunzi alipata _____ya muwa huo
a. Thumuni
b. Subui
c. Tusui
d. Ushuri
11. ______ni malipo ya kwanza ya kununulia kitu
a. Arbuni
b. Kiangaza macho
c. amana
d. Kishika mkono
12. Ajuza alimwambia mjukwe aende kanisani bila kuchelewa ,kauli hii katika usemi halisi itakuwa
a. Enda kanisani bila kuchelewa.”ajuza alimwambia mjukwe
b. “Enda kanisani” bila kuchelewa. Mjukuu alimwambia Ajuza
c. “Mjukuu aliambiwa na ajuza “enda kanisani bila kuchelewa
d. “Enda kanisani bila kuchelewa ,”Ajuza alimwambia mjukuwe
13. Mwanana alikimbia polepole . Neno polepole ni
a. Kiashiria
b. Kielezi
c. Kihusishi
d. Kitenzi
14. Sauti inayorejelea pindi tu mtu apigapo kelele karibu na mlima huitwa
a. Mvangwi
b. Makoka
c. Mangi
d. Twasira
15. Opondo anaishi kaskazini mashariki mwa kina otoyo kwa hivyo kina otoyo wanaishi
a. Mashariki
b. Kaskazini magharibi
c. Kusini magharibi
d. Kusini mashariki

kiswahili revision papers