3.1. Kifungu cha Tatu Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 10:23 AM by Maurice Nyamoti   [ updated Aug 1, 2015, 10:28 PM ]

Soma kifungu Kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.


Aliamka alfajiri__1 ili niweze kufika hapa nilipo kwa wakati __2. Si kwamba kuamka nyakati __3 ni kawaida __4. La__5. Niliamka nifike hapa ili niweze k uchakura ukurasa katika harakati __6 mwishomwisho za maandalizi kwa mitihani .Hakika mtihani__7 ninaoufanya__8 sasa __9 si kwa hamu na ghamu tu,__10 kwa moyo wangu wote. Naam , hayawi hayawi __11, siku yenyewe na wakati __12 ndio huu u mefika na karatasi ndiyo hii hapa mbele yangu .Kazi sasa ni __13 mtihani na kupiga __14 au kuanguka na__15___.

1.
a. Asubuhi
b. Tena
c. Mbichi
d. Huo
2.
a. Zifaazo
b. Ufaawo
c. Lifaalo
d. Kufaako
3.
a. Hiki
b. Huyo
c. Yule
d. Hizi
4.
a. Kwangu
b. Yangu
c. Kwako
d. Yake
5.
a. Haswa
b. Hasa
c. Hasha
d. Hata
6.
a. Kwa
b. Za
c. Mwa
d. La
7.
a. Huku
b. Kule
c. Huu
d. Hizi
8.
a. Humu
b. Kwa
c. Hivi
d. Hivyo
9.
a. Nimeusuburi
b. Nimeisubiri
c. Nimeyasubiri
d. Nimezisubiri
10.
a. Ile
b. Mbali
c. Bali
d. Hali
11.
a. Yanakuwa
b. Kunakucha
c. Kunaonekana
d. Huwa
12.
a. Mwenyewe
b. Yenyewe
c. Wenyewe
d. Lenyewe
13.
a. Kuuraruwa
b. Kuipasi
c. Kuupita
d. Kuyapita
14.
a. Mbinja
b. Kidogo
c. Usukani
d. Bisimilahi
15.
a. Kujiumiza
b. Kujikwaa
c. Kulaumu
d. kujilaumu

kiswahili revision papers