1.3. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Tatu - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:01 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali 1-10


Mafunzo ya kuimarisha maadili katika jamii ni muhimu. Kinyume na hapo awali, sasa maadili ya jamii zetu yanazoroteka kwa kasi sana kiasi cha kushangaza. Mwingiliano mwingi kati ya mataifa ya Kiafrika na ya kigeni unaweza kuleta upungufu wa maadili. Watu wengi hufikiria kuwa upotovu wa maadili ndio ustaarabu ufaao. Kusifu na kuziiga nyendo mbaya huchangia upalilizi wa uozo wa tabia. Hali hii inaweza kuzifuja nchi hizi.
Ni dhahiri shahiri kuwa umaskini wa nchi umewafanya vijana kwa wazee kutamani na kuzitafuta njia zamkato za kujitajirisha. Kwa kuingiwa na tamaa nyingi, wao huanzisha miradi ya kifisadi. Watu hao hufanya juu chini kutafuta mlanya ya kujipenyeza fedha. Wao hufanya haya bila ya kujali madhara yanayoletwa na hizo pilkapilka zao. Hongo huzidi kuendelezwa ili kuficha hizo njama ambazo huwa hatari kwa usalama wa nchi na watu wake.
Tamaa ikithiri mpaka, bongo za fisadi hao hazitulii bali huenda kwa haraka isiyomithilika. Watu hujikweza wakitaka kuwafikia na kuwapita waliowatangulia kiuchumi. Mathalani, watu ambao hivi majuzi walionekana hoi ama atu wa kawaida, ghafla huonekana watu wa kuishi kitajiri huku akijijengea majumba ya ghorofa katika mitaa ya kifahari. Kama hali hiyo ingeletwa na kushukiwa na nyota ya jaha, ungeelewa. lakini kama utajiri huo unatokana na kufurisha mifuko kwa kulete shoti ofisini, wakitumia wizi wa kalamu au kula mlungula, itabidi utiliwe shaka na kulaaniwa. Vijana ambao ndio wajenzi wa taifa taifa wa leo na kesho wanapaswa kuvipuuza vitendo hivyo kwa sababu vinadhalilisha utu wa jamii.
Serikali nyingi za Kiafrika hutafuta  mikakati ya kukabiliana na ufisadi ili ziimarishe maadili. Mojawapo ya hiyo mikakati ni hatua ya serikali ya kuwahimiza wananchi kujaza fomu kuonyasha jumia ya rasilimali zao. Hata hivyo wahusika katika ufisadi hutafuta vizingiti vya kuzizuia juhudi hizo za serikali.
Ni bayana kuwa mtu hawezi kushindabna na mkono mrefu wa serikali. Juhudi za kukomesha vituko nya ufisadi zimeanza kuzaa matunda. Tayari vielezo vya kupambana na ufisadi vimeanza kujidhihirisha vyenyewe. Hivi majuzi vituko vya kujenga nyumba hafifu hapa nchini vilifuatilia unyounyo na wahusika kufunguliwa mashtaka; hasa baada ya watu kupoteza maisha yao na wengine kulemazwa walipoangukiwa na nyumba hizo. Kwa mfano, watu waliodai kuwa watajenga ghorofa tatu. Walibadili nia na kujenga ghorofa zaidi. Walifanya hivyo baada ya kupata vibali vya pembe za chaki. Isitoshe, kwa kutaka kutajirika haraka walinunua na kuvitumia vifaa duni kinyume na kanuni za uhandisi. Mambo kama haya hujitokeza katika nchi nyingi barani Afrika. nchi hizi sasa zimeamka na kukaza kamaba katika kuupinga ufisadi huu. Ikumbukwe kuwa ufisadi unaotokana na ukosefu wa maadili no hatari kubwa kwa nchi yoyote ile. Mienendo kama hii hufuja nchi husika. Ni vyema kuepuka tabia hizi kama mtu aepukavyo ugonjwa wa kuambukiza.

 1. Nchi zetu zinazidi kuharibiwa na:
  1. kufuata ustaarabu wa kigeni na kuppuza maadili
  2. wananchi wapendao maadili ya mataifa yao
  3. vijana wanaoigiza maadili yafaayo
  4. kutoelewa vizuri maana ya maadili
 2. Chagua maelezo yaloyo sawa kulingana na aya ya pili.
  1. njama za ufisadi zinailetea nchi matatizo
  2. usalama wa nchi hautegemei pilkapilkja za fisadi
  3. maskini wote wanatafuta njama za kujitajirisha kifisadi
  4. njia za mkato zatajirisha nchi upesi
 3. Ushahidi kuwa ufisadi upo ni:
  1. kuwapo na kuziiga nyendo za kigeni
  2. kupatikana ka haraka ka mambo ya kifahari
  3. kujenga majumba makubwa na ya kifahari katika mitaa bora
  4. kuonekana kwa mabaliko ya ghafla kiuchumi kwa waliotajika
 4. Utajiri unaotiliwa shaka ni ule:
  1. wa kuigwa na watu wote
  2. usio na wizi wa kalamu
  3. wa njama za uharibifu
  4. upendwao na vijana nchini
 5. Kushukiwa na nyota ya jaha ni sawa na:
  1. mchezo wa bahati nasibu
  2. kupewa zawadi kwa kushinda
  3. kupata ka haraka
  4. kubahatika kihalali
 6. Kulingana na taarifa hii, mawazo ya fisadi:
  1. yanaimarisha nchi kiuchumi kwa kutajirika
  2. hayazingatii utamaduni wa wote
  3. hutafuta njia mbalimbali za kujitajirisha
  4. yanatamani maadili ya watangulizi wao
 7. Upalilizi wa uozo wa tabia huendelezwa kwa:
  1. kupenda na kuzifuata tabia za kifisadi
  2. kufikiria tu juu ya upotovu wa maadili
  3. kusifu na kuzifuata nyendo zote za kigeni
  4. mwingiliano wa binadamu katika ustaarabu
 8. Madhara makuuu yanayoweza kupata jamii ya kifungu ni:
  1. vijana kuupenda na kuuiga utamaduni wa kigeni
  2. umasikini mkubwa unaorudisha nchi nyuma kiuchumi
  3. watu kuingilia njama za kifisadi kwa kutaka kutajirika
  4. maangamizi yanayoletwa na watu wenye njama za kifisadi
 9. Mwandishi wa taarifa hii ana msimamo kuwa:
  1. Ustaarabu wote wa kigeni unapotosha maadili
  2. maadili yatafaulishwa na vijana na serikali husika
  3. uigaji wa nyendo za kigeni unapaswa kuzuiwa
  4. ujenzi wa ghorofa duni na njama za kifisadi zimezidi
 10. kifungu hiki kinaweza kufupishwa kwa kutumia methali:
  1. mwacha mila ni mtumwa
  2. mia nawe hafi nawe ila mzaliwa  nawe
  3. tamaa mbele mauti nyuma
  4. vyote ving'aavyo si dhahabu
fasihi