1.4. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Nne - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:05 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Masika alikuwa mwanafunzi mgeni katika shule ya Kiwesero. Alikuwa katika darasa la tatu. Hakuna aliyejua alikotoka. Isitoshe hakucheza wala kushirikiana na watoto wenzake. Wakato wa chakula cha mchana, aliketi chini ya mti pake yake. Mawazo yake yalikuwa mbalimbali. Daima dawamu alisinzia darasani. Lionekana mgonjwa au mchovu.
Baadhi ya wanafunzi walimfanyia mzaha kwa kuimba "masika ni mchafu kama ufagio, masika anaogopa maji!" maneno hayo yalimchoma sana Masika, Masero alimwonea huruma Masika. "Masika, kwa nini hutaki kucheza nasi?" Masero alimuuliza akimpa andazi.
"Asante Masero, ningependa kucheza nanyi lakini mimi ni maskini hohehahe, Viatu vyangu vimeraruka, mavazi yangu ni matambara. Nimelala njaa," masika alimjibu kwa haya.
"Wazazi wako wanofanya kazi gani?" Masero aliuliza. "Baba alikuwa mkulima mama alikuwa mfanyabiashara wa samaki."Halafu?" Masero alikuwa na hamu ya kujua zaidi masika alimweleza yote yaliyowapata.
"Zamani tuliishi sehemu za Molo. Nyumba yetu alichomwa baada ya uchaguzi mkuu. Tulifanikiwa kutoroka lakini bila chochote. Sasa tunaishi katika kambi ya wakimbizi tunategemea wasemaria wema. Hatuna maji wala chakula cha kutosha. Hema letu ni dogo sana. Tunatumia taa ya koroboi tui, "Masika alisema.
"Nina vitabu, nguo na viatu ambavyo situmii. Nitawaomba wazazi wangu ruhusa ya kukupa," Masero alisema. "Utakuwa umenifaa. Nayachukia haya matambara, "alisema.
Jioni hiyo, Masero aliandamana na masika hadi kwao. "Mama, huyu rafiki yangu anaitwa Masika, ningependa tumsaidie,"Masero alimmsihi mzazi wake. Masika alimweleza mama Masero matatizo yao."Wakati mwingine tunalala njaa tukipigwa na baridi,"alisema.
"Pole sana, masika, una bahati kwa kuwa unatoshana na Masero. Nitakugawia mavazi yake, Uko huru kuja hapa kuoga na kupata ckakula cha mchana. Mwambie baba yako aje tukutane"
Tangu siku hiyo, maisha yalikuwa afadhali Wazazi wa masika alihamia katika boma la kina Masero, walipewa chumba cha mfanyakazi. Ingawa kulikuwa kidogo, kilikuwa afadhali kuliko kambi ya wakimbizi.
Kwa kweli, Mungu hamsahau mja wake, Kwani baada ya miezi miwili, mamake Masero aliwatafutia wazazi wa Masika kazi nzuri sana, haakuamini macho yao, maisha ya kina masika hohehahe yalibadilika ghafla kama umeme, yote hayo kwa sababu ya urafiki kati ya Masika na Masero.
 1. Kwa nini wanafunzi wa shule ya kiwesero hawakujua alikotoka?
  1. Alikuwa hajui kuongea
  2. Alikuwa mdogo sana na kwa hivyo hakuweza kuwaelezea
  3. Hakushirikiana na yeyote
  4. Aliketi chini ya mti peke yake
 2. Mawazo yake yalikuwa mbali, inamaanisha
  1. Aliketi mbali na darasa kila wakati
  2. Alikuwa na kasoro akilini mwake
  3. Alifikiri wanafunzi wenzake hawampendi
  4. Hakuyatilia maanani yote yaliyosemwa darasani
 3. Masero alikuwa nani?
  1. Rafiki yake Masika
  2. Mwanafunzi waliosoma katika darasa moja
  3. Mwanafunzi waliosoma katika shule moja
  4. Jirani yake Masika
 4. Kitendo cha Masero ni cha mtoto
  1. Mtukutu
  2. Mwerevu
  3. Mwenye utu
  4. Mtulivu
 5. Kulingana na taarifa hii, ni sentensi ipi ambayo ni sahihi?
  1. Wazazi wa Masika walikuwa wakulima
  2. Masika alikuwa maskini hohehahe
  3. Masika alisinzia darasani daima dawamu
  4. Mamake Masero ni mwanamke mwenye huruma
 6. Bila shaka, Masero alimwwuliza masika maswali mara kwa mara kwa sababu?
  1. Alikuwa anataka kumsaidia
  2. Alikuwa na tabia ya udaku
  3. Alimwonea huruma sana
  4. Hajawahi ona maskini hohehahe kama masika
 7. Kulingana na taarifa hii, mamake Masero
  1. Anawatesa sana kina Masika
  2. Alikuwa mzuri kupita kiasi na pia mwenye huruma
  3. Alikuwa na shida nyingi sana
  4. Alikuwa mkwasi
 8. Tangu siku hiyo, maisha yalikuwa afadhali
  Ni siku gani hii inayozungumziwa?
  1. Masika alipoenda kwa kina Masero
  2. Masika alipoenda shuleni
  3. Wazazi wa Masika walipopata kazi
  4. Wazazi wa Masika walipokutana na Mamake Masero
 9. Baada ya kupata kazi, wazazi wa masika
  1. Waliendelea kuishi kwa kina Masero
  2. Walirudi kwao Molo
  3. Walitafuta makao yao, mapya
  4. Walirudi katika kambi
 10. Taarifa hii inaweza kufupishwa kwa kutumia methali
  1. Mungu si Athumani
  2. Chanda chema huvishwa pete
  3. Mtegemea nundu haachi kunona
  4. Fuata nyuki ule asali
fasihi