1.7. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:18 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Kijana Matata alizaliwa katika kijiji cha Mashaka mwaka wa elfu moja kenda mia tisini na tatu. Kama ilivyo kawaida katika mila na desturi za Waafrika,mwana ni tunu kutoka kwa Mola. Wengi wa wanakijiji walifurahia kuingia kwa Matata duniani. Hali hii ilichochewa na idhibati ya wanawaliokuwa wamezaliwa hapo awali. Wengi baada ya kupata kisomo waliishia kuwa watatuzwa shida kemkem zilizo wakumba wakazi wa eneo lao. Walitarajia Matata afuate nyayo za watangulizi wake na kuyafanya maisha ya wakazi kuwa rahisi lakini hivyo sivyo mambo yalivokuwa.

          Baada ya Matata kujiunga na shule ya msingi, masomo yake yaliendelea vizuri hadi pale alipofika darasa la saba. Alianza kuingiwa na uchu wa pesa. Aliamua kuwa akiwasaidia walanguzi wa dawa za kulevya ambaotayari walikuwa wamebadilisha mbinu za kusafirisha dawa hizo. Waanguzi hawa waliamua kumtumia Matata ili kukwepa mkono mrefu wa sheria. Wao walifanya hivi kwa kuwa sio rahisi kwa maafisa wa polisi kudadisi au kushuku mwanafunzi.  Kufuatia hali hii kamishna wa polisi aliwahimiza walimu wakuu wa shule za msingi na upili kuwa makini na kufuatilia mienendo ya wanafunzi wao kila wakati.

          Kutokana na utumizi mingi wa dawa za kulevya, mwalimu mkuu wa shule aliyosomea Matata aliamua kumwalika mshaurinasaha ili kuwahutubia wanafunzi. Alianza,”Wanafunzi ambao wako shuleni hivi sasa ndio tegemeo la taifa hili siku zijazo na itakuwa hasara kubwa iwapo watajiingiza katika lindi la matumizi ya dawa za kulevya. Itakuwa sio sawa kwetu kulinyamazia suala hili, hivyo basi ni wajibu wetu kulivalia njuga na kutumia kila mbinu ili kuokoa maisha ya wanafunzi. Tusipofanya hivi udongo utakauka na itakuwa vigumu kuuwahi.

          Walimu ni lazima muwe makini na mandhari  yanayozunguka shule na msisite kupiga ripoti katika kituocah chochote cha polisi iwapo mtagundua harakati zozote za biasharahiyo haramu zikiendeshwa. Kumbukeni kunyamaza kwenu  kutakuwa sawa na kuchangia katika uovu huo. Daw za kulevya ukizizoea zinakuwa ni saratani. Athari zake ni nyingi hususani kwa  mwanafunzi kwa matokeo yake hudorora  katika tamrini za madarasani,utovu wa nidhamu na pia dawa hizi huathiri  afya ya mtumiaji. Walio katika uraibu huu wakome  mapema kwa kuwa usipoziba ufa utajenga ukuta.”

          Matata alikuwa ametega masikio ndi! Kwa kuwa walimu walikuwa wameona yote yaliyosimuliwa na mshaurinasaha kutoka kwa Matata; walimwita ili kumdadisi kiasi.walishangaa walipotumbukiza mkono kwenye mkoba wa Matata na kupata pakiti kadhaa za dawa za kulevya. Papo hapo walimketisha chini ili kubaini mbivu na mbichi. Hapo Matata akawafungulia moyo na kuwaeleza walimu wake vile ambavyo amekuwa akitumiwa na walanguzi wa dawa za kulevya. Walimu walikenua midomo yao wasiweze kuamini kuwa walikuwa wamefeli katika majukumu yao iwapo kwa muda huo wote hawakuwahi kugundua kuwa Matata alikuwa mraibu wa mihandarati. Matata aliamua kubadilika huku akisadiki kuwa mui huwa mwema.

1.    Wakazi wa kijiji cha Mashaka walifurahia kuzaliwa kwa Matata kwa kuwa__

a.     Mtotoni tunu kutoka kwa mola

b.    Wengi wa wana waliozaliwa hapo awali walichangia katika shida zao.

c.     Matata alikuwa mwana wa kipekee aliyekuwa na kipawa cha kipekee.

d.    Alionekana kuwa matatuzi wa shida nyingi zilizowakumba wakazi wa eneo hilo.

2.    Kwa nini walanguzi wa mihandarati waliamua kumtumia Matata katika biashara yao?

a.     Matata alikuwa amependezwa na kazi hiyo tangu  alipozaliwa

b.    Watumizi wengi wa dawa za kulevya walikuwa ni wanafunzi

c.     Lengo lao lilikuwa ni kukwepa mkono mrefu wa sheria

d.    Matata mwenyewe aliamua kuwa akiwasaidia katatika biashara hiyo.

3.    Msemo “uzee hula ujana” unajitokeza pale,

a.     Wanafunzi waambiwa kuwa wao ndio tegemeo la taifa letu siku zijazo.

b.    Kamishna wa polisi anawataka walimu wakuu wawe waangalifu na mazingira ya shuleni.

c.     Mwalimu mkuu anamwita mshaurinasaha kuzungumzia suala la mihadarati.

d.    Watoto wengi wa mtaa wa Mashaka walinukia kuwa watatuzi wa shida nyingi

4.    Ni nini maana ya ujumbe uliopigiwa kistari?

a.     Udongo mgumu haukandiki kwa urahisi

b.    Wanafunzi wasipotilia maanani bidii shuleni watakuwa wakifanya kazi za udongo

c.     Mwanafunzi anayetumia mihadarati ni sawa na nyumba ya udongo

d.    Walimu wakichelea kukabiliana na tatizo la mihadarati,kizazi kitakuwa kimepotea

5.    Athari za dawa za kulevya kwa mwanafunzi kulingana na makala haya ni___

a.     Kusinzia darasani,kuchoka ovyo na utovu wa nidhamu.

b.    Utovu wa nidhamu,kufeli mitihani na kuchoka.

c.     Kuugua,kufeli mitihani na utovu wa nidhamu

d.    Kuugua,kusinzia darasani na utovu wa nidhamu

6.    Kichocheo kikuu cha mwalimu mkuu kumwalika mshaurinasaha kilikuwa___

a.     Yeye hakutaka kulaumiwa na kamishna wa polisi atialikuwa ameshindwa na majukumu yake

b.    Hakuwahi kulizungumzia suala la dawa za kulevya

c.     Aliwashuku baadhi ya wanafunzi kuwa walnguzi wa mihadarati

d.    Utumizi mkubwa wa mihadarati katika eneo husika.

7.    Kwa nini walimu walimketisha Matata chini?

a.     Ili kubaini dawa mbivu na mbichi zilizopatikana mfukoni mwake.

b.    Ili kumaizi chimbuko na asili ya mihadarati  iliyopatikana mfukoni mwake

c.     Ili waweze kujionea jinsi dawa za kulevya zilivyo kuwa.

d.    Ili wachunguze iwapo kulikuwa  na mwalimu yeyote aliyehusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya.

8.    Walimu walikenua midomo. Hii ilikuwa ishara ya

a.     Kukasirika

b.    Kufurahi

c.     Kushangaa

d.    Kuridhika

9.    Kilichomfanya Matata ashiriki katika biashara hii haramu ni___

a.     Urafiki na wandani walanguzi wa mihadarati

b.    Tama ya pesa

c.     Malezi mabaya

d.    Kutomakinika kwa walimu

10.  Anwani ifaayo makala haya ni___

a.     Siku za mwizi ni arobaini

b.    Utumizi wa dawa za kulevya

c.     Jukumu la waalimu katika kukabiliana na mihadarati

d.    Wakazi wa Mashaka wajutia vitendo vya Matata

fasihi