1.8. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Nane - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:21 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Raia ni mtu mwenye haki za kisheria kutokana na kuzaliwa au kujiandikisha katika taifa Fulani. Haki hizo za kisheria zinamwezesha kushiriki katika shughuli zote za taifa hilo. Kuna raia mwema na raia mbaya. Raia mwema ana roho safi. Ni mwungwana, mwadilifu na mhisani mkubwa. Daima yuko tayari kujitolea na kutoa alicho nacho kwa ajili ya taifa lake na raia wengine. Ni mtiifu na si mwasi wa kanuni na sheria zozote za nchi. Naye huwachukia waovu yao. Na huyo ndiye mzalendo, raia mwema.
Raia mwema ana haki na wajibu wa kulinda nchi yake kutokana na uhalifu na ufisadi wa aina yoyote. Hatoi rushwa wala hahongeki. Hafichi maovu wala hatendi maovu. Kila tendo baya alionalo hachelei kuwadokeza wengine na kuwaarifu polisi wa usalama. Raia mwema ni jicho la taifa, sikio la taifa na ni sauti ya wapenda haki. Raia mwema akitumwa kuenda kutenda haki, hachelei. Akiangaziwa akatende maovu husita. Siku zote huzingatia na kujikumbusha maadili huku akisema,”nitatenda haki daima,maovu kwangu ni mwiko!”
Njia bora kukomesha maovu na ufisadi katika nchi kusimama juu ya kiduta cha ukweli na uaminifu. Nchi ya watu wasio waaminifu, haiwezi kukutetae wala kukutendesha haki. Tushirikiane, sisi kwa sisi pamoja na walinda usalama, ili tumalize adui, rushwa, ufisadi, ujambazi, wizi, ubakaji, uongo, ugaidi, uzembe,unyakuzi na chuki.
1.       Raia ni
a.       Mkazi mwenye haki kisheria katika nchi yake
b.      Si mzalendo ni mlowezi
c.       Si rahisi raia
d.      Anashiriki katika shughuli zote za nchi
2.       Sifa ya raia mbaya ni
a.       Ufisadi
b.      Uungwana
c.       Utiifu
d.      uzalendo
3.       Mzalendo ni raia
a.       Mlowezi wa taifa
b.      Mbepari wa kujitakia makuu
c.       Mfisadi asijali masilahi yaw engine
d.      Anayejitolea mhanga kwa ajili ya taifa
4.       Raia mwema akiyaona matendo maovu
a.       Huogopa kuyafichuo
b.      Huyaficha
c.       Huyafichua
d.      Huarifu vyombo vya habari
5.       Kutoa habari kwa polisi ni katika jumla ya:-
a.       Kuendeleza chuki
b.      Uraia mwema
c.       Kuangamiza nchi
d.      Utovu wa uzalendo
6.       Matendo maovu yanaweza kutokomezwa nchini mwetu na nani?
a.       Sisi wenyewe
b.      Polisi
c.       Washikadau
d.      wanajeshi
7.       Neno “mwiko”limtumika katika habari hii kwa maana ya
a.       Kijiko kikubwa
b.      Upawa wa kukorogea mlo
c.       Haramu au baili
d.      mwisho
8.       Taarifa hii inasema kwamba mtu anapokataa kusema ukweli ama kuficha maovu, basi ajue kwamba
a.       Anazorotesha maovu katika jamii
b.      Anadumisha haki za nchi
c.       Anawasaidia polisi kutetea haki
d.      Anachangia ufisadi nchini
9.       Sisi kwa sisi maana yake ni
a.       Nyumbani kwetu sisi
b.      Sisi wenyewe miongoni mwetu
c.       Wengine bila sisi
d.      Sisi na polisi wa usalama
10.   Madili ya makala haya ni kwamba
a.       Mjenga nchi ni mwananchi na mvunja nchi ni mwananchi
b.      Nahodha wengi chombo huenda mrama
c.       Raia ni bendera hufuata viongozi
d.      Siku za mwizi ni arubaini
fasihi