1.5. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:07 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Japo watu wanaovuta bangi hawamiini kwamba ina madhara yoyote kwa afya yao. Utafiti wa juzi wa kisayansi umethibitisha kwamba bangi husababisha shida nyingi za kiafya
Kulingana na shirika la serikali kukabiliana na dawa za kulevya, NACADA idadi ya watu wanaovuta bangi nchini imekuwa ikipanda licha ya juhudi za kukomesha utumiaji wa dawa hizo.
Wanasayansi wanasema madhara yanayotokana na uvutaji bangi hudumu kwa mda mrefu sana ikilinganishwa na dawa zingine za kulevya, kama vile tumbaku.
Baadhi ya athari za bangi kwa mvutaji ni shida ya kuona kusikia au hisia kififia fikira kutatizika, shida za moyo na damu kwenda kasi mwilini msukumo wa mawazo, hofu na taharuki.
Bangi huwa na kemikali moja amabayo hutawanyisha seli za ubongo na kumfanya mvutaji kuonekana kama kamba amerukwa kichwa kadhalika, bangi hukatiza mawasiliano kati ya ubongo na misuli katika sehemu zote za mwili.
Hii ndiyo sababu mtu akivuta bangi anaweza kufanya kazi ambayo ingefanya na zaidi ya watu watatu kwa sababu ubongo huchanganyikiwa na kumfanya mtu kuhisi kwamba ana nguvu.
Dakika tatu au tano baada ya mtu kuvuta bangi, moyo wake huanza kupiga kwa haraka na kumweka katika hatari kubwa ya kukubwa na mshtuko wa moyo
Unapovuta bangi hata mara moja au mbili kwa wiki, mdomo na koo huanza kuwasha na kukufanya kuanza kukohoa kila mara.
Kwa mujibu wa wanasayansi watu wanaovuta bangi hukumbwa na shida za kupumua kama vile mtu anayevuta tumbaku
Kwa mujibu wa wanasayansi, bangi huwa na viwango vya juu vya kemikali zinazosababisha kansa kuliko tumbaku.
Athari zingine mbaya zinazotokana na uvutaji bangi ni kwamba bangi humfanya mvutaji kupungukiwa kinga ya mwili. Hivyo mtu anayevuta bangi yumo katika hatari kubwa ya kukumbwa kila wakati na magonjwa mbalimbali.
Utafiti unaonyesha kwamba watoto wanaozaliwa na wazazi wanaovuta bangi hukumbwa na shida nyingi za kiakili na wengi wao hawafanyi vyema masomoni.
Katika hali zingine, uvutaji bangi umesababisha madhara mabaya zaidi kama vile kuwa wazimu. Ikiwa wewe ni mmoja wa wanaovuta bangi, itakuwa muhimu kwako kwenda vituo vya afya kupata ushauri jinsi unavyoweza kuepukana na uraibu wa kuvuta bangi
 1. Inaaminiwa kuwa watu wanaovuta bangi
  1. Wanaelewa madhara bangi huwaletea kwa afya zao
  2. Hawaamini kwamba bangi ina madhara yoyote
  3. Wanajua bangi husababisha shida nyingi
  4. Afya zao huzorota mara kwa mara
 2. Idadi ya watu wanaovuta bangi nchini
  1. Inaongezeka licha ya wavutaji bangi kukomeshwa
  2. Inapungua kwa kuwa NACADA inakabiliana na wavutaji bangi
  3. Imewapendeza sana NACADA
  4. Inapanda kwa sababu wavutaji bangi hwana kazi za kufanya
 3. Chagua jawabu lililo sahihi zaidi
  1. bangi iko na madhara sawasawa na tumbaku
  2. wavutaji bangi huwa na kinga mwilini
  3. wavutaji bangi wamo hatarini sana
  4. wavutaji bangi wanaweza kuepukana na uraibu wa kuvuta bangi
 4. Ni nini hasa kinachomfanya mvutaji bangi kuonekana kama kwamba amerukwa kichwa?
  1. shida ya kuona, kusikia au hisia kufifia
  2. shida za moyo na damu kwenda kasi mwilini 
  3. mshtuko wa moyo
  4. seli za ubongo kuharibiwa na kemikali moja
 5. Kulingana na taarifa hii, maana ya uvutaji bangi hudumu kwa mda mrefu sana ni
  1. Afadhali kuvuta dawa zingine za kulevya kuliko bangi
  2. Madhara ya wavutaji bangi hukawia sana mwilini kabla ya kutoka kikamilifu
  3. Tumbaku haina madhara yoyote
  4. Pindi tu ukianza kuvuta bangi, itakuwa shida sana kuacha kuvuta kwa sababu utakuwa umezoea tayari
 6. Mwandishi wa taarifa hii anaamini kuwa mshtuko wa moyo husababishwa na
  1. Moyo kupiwa kwa haraka mtu anapovuta bangi
  2. Mvutaji bangi anapoifanya kazi ambayo ingefanywa na watu watatu
  3. Mvutaji bangi anapoanza kukohoa
  4. Upungufu wa kinga mwilini
 7. Bila shaka, uvutaji tumbaku una madhara gani?
  1. Tumbaku husababisha kansa
  2. Kupungukiwa kinga ya mwili
  3. Shada za kupumua
  4. Kuwa wazimu
 8. Utafiti uliofanywa mwaka uliopita ulionyesha kwamba
  1. Wavutaji tumbaku hawawezi ugua kansa
  2. Tumbaku haina kiwango cha juu cha kemikali
  3. Afadhali watu avute tumbaku kuliko bangi
  4. Wavutaji bangi wamo hatarini ya kuugua kansa kuliko wanaovuta tumbaku
 9. Mvutaji bangi anaweza kuepukana na uraibu wa kuvuta bangi
  1. Akienda kanisani mara kwa mara
  2. Akipata ushauri katika kituo cha afya
  3. Akia mgonjwa kisha atibiwe
  4. Akipelekwa hospitalini
 10. Kichwa kinachofaa zaidi kwa taarifa hii ni
  1. uvutaji bangi
  2. madhara ya bangi
  3. uvutaji tumbaku
  4. kukabiliana na dawa za kulevya
fasihi