1.1. Kifungu cha Kujibu Maswali Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 3:55 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali 1-10


Kijana matata alizaliwa katika kijiji cha Mashaka mwaka wa elfu moja kenda mia tisini na tatu. Kama ilivyo kawaida katika mila na desturi za Waafrika, mwana ni tunu kutoka kwa Mola. Wengi wa wanakijiji walifurahia kuingia kwa matata duniani. Hali hii ilichochewa na idhibati ya wana waloikuwa wamezaliwa hapo awali. Wengi baada ya kupata kisomo waliisha uwa watatuzwa shida kemkem zilizowakumba wakazi wa eneo lao. Walitarajia Matata afuate nyayo za watangulizi wake na kuyafanya maisha ya wakazi kuwa rahisi lakini hivyo sivyo mambo yalivyokuwa.
Baada ya Matata kujiunga na shule ya msingi, masomo yake yaliendelea vizuri hadi alipofika darasa la saba. Alianza kuingiwa na uchuwa pesa. Aliamua kuwa akiwasaidia walanguzi wa dawa za kulevya ambao tayari walikuwa wamebadilisha mbinu za kusafirisha dawa hizo. Walanguzi hawa waliamua kumtumia Matata ili kukwepa mkono mrefu wa sheria. Wao walifanya hivi kwa kuwa sio rahisi kwa mafisa wa polisi kudadisi au hata kushuku mwanafunzi. Kufuatia hali hii kamishna wa polisi aliwahimizi walimu wakuu wa shule za msingi na upili kuwa maakini na kufuatilia mienendo ya wanafunzi wao kila wakati
Kutokana na utumizi mwingi wa dawa za kulevya, mwalimu mkuu wa shule aliyosomea Matata aliamua kumwalika mshaurinasahe ili kuwahutubia wanafunzi. Alianza, “Wanafunzi ambao wako shuleni hivi sasa ndio tegemeo la taifa hili siku zijazo na itakuwa hasara kubwa iwapo watajiingiza katika lindi la matumizi ya dawa za kulevya. Itakuwa sio sawa kwetu kulinyamazia suala hili, hivyo basi ni wajibu wetu kulivalia njuga na kutumia kila mbinu ili kuokoa maisha ya wanafunzi. Tusipofanya hivi udogo utakauka na itakuwa vigumu kuuwahi.
Walimu ni lazima muwe makini na mandhari yanayozunguka shule na msisite kupiga ripoti katika kituo chochote cha polisi iwapo mtagundua harakati zozote za biashara hiyo haramu zikiendeshwa. Kumbukeni kunyamaza kwenu kutakuwa sawa na kuchangia katika uovu huo. Dawa za kulevya ukizizoea zinakuwa ni saratani. Athari zake ni nyingi hususani kwa mwanafunzi kwa matokeo yake hudorora katika tamrini za madarasani, utovu wa nidhamu na pia dawa hizi huathiri afya ya mtumiaji. Walio katika uraibu huu wakome mapema kwa kuwa “usipoziba ufa utajenga ukuta”.
Matata alikuwa ametega masikio ndi! Kwa kuwa walimu walikuwa wameona yote yaliyosimuliwa na mshaurinasaha kutoka kwa Mataata; walimwita ili kundadisi kiasi. Walishangaa walipotumbukiza mkono kwenye mkoba wa Matata na kupata pakiti kadhaa za dawa za kulevya. Papo hapo, walimketisha chini ili kubai mbivu na mbichi. Hapo Matata akawafungulia moyo na kuwaeleza walimu wake vile ambavyo amekuwa akitumiwa na walanguzi wa dawa za kulevya. Walimu walikenue midomo yao wasiweze kuamini kuwa walikuwa wamefeli katika majukumu yao iwapo kwa muda huo wote hawakuwahi kugundua kuwa Matata alikuwa mraibu wa mihadarati. Matata aliamua kubadilika huku akisadiki kuwa mui huwa mwema

1. Wakazi wa kijiji cha mashaka walifurahia kuzaliwa kwa Matata kwa kuwa,
A. Mtoto ni tunu kutoka kwa Mola
B. Wengi wa wana waliozaliwa hapo awali walichangia katika kutatua shida zao
C. Matata alikuwa mwana wa kipekee aliyekua na kipawa cha kipekee
D. Alionekana kuwa mtatuzi wa shida nyingi zilizowakumba wakazi wa eneo hilo
2. Kwa nini walanguzi wa mihadarati waliamua kumtumia Matata katika biashara yao?
A. Matata alikuwa amependezwa na kazi hiyo tangu alipozaliwa
B. Watumizi wengi wa dawa za kulevya walikuwa ni wanafunzi
C. Lengo lao lilikuwa ni kukwepa mkono mrefu wa sheria
D. Matata mwenyewe aliamua kuwa akiwasaidia katika biashara hiyo
3. Msemo “Uzee hula ujana” unajitokeza pale
A. Wanafunzi waambiwa kuwa wao ndio tegemeo la taifa letu la siku zijazo
B. Kamishna wa polisi anawataka walimu wakuu wawe waangalifu na mazingira ya shuleni
C. Mwalimu mkuu anamwita mshaurinasaha kuzungumzia suala la mihadarati
D. Watoto wengi wa mtaa wa Mashaka walinukia kuwa watatuzi wa shida nyingi za wakazi
4. Ni nini maana ya ujumbe uliopigiwa kistari?
A. Udongo mgumu haukandikiki kwa urahisi
B. Wanafunzi wasipotilia maanani bidii shuleni watakuwa wakifanya kazi za udongo
C. Mwanafunzi anayetumia mihadarati ni sawa na nyumba ya udongo
D. Walimu wakichelea kukabiliana na tatizo la mihadarati, kizazi kitakuwa kimepotea
5. Athari za dawa za kulevya kwa mwanafunzi kulingana na makala haya ni
A. Kusinzia darasani, kuchoka ovyo na utovu wa nidhamu
B. Utovu wa nidhamu, kufeli katika mitihani na kuchoka
C. Kuugua, kufeli mitihani na utovu wa nidhamu
D. Kuugua, kusinzia darasani na utovu wa nidhamu
6. Kichocheo kikuu cha mwalimu mkuu kumwalika mshaurinasaha kilikuwa
A. yeye hakutaka kulaumiwa na kamishina wa polisi ati alikuwa ameshindwa na majukumu yake
B. Hakuwahi kulizungumzia suala la dawa za kulevya
C. Aliwashuku baadhi ya wanafunzi kuwa walanguzi wa mihadarati
D. Utumizi mkubwa wa mihadarati katika eneo husika
7. Kwa nini walimu walimketisha Matata chini?
A. Ili kubaini dawa mbivu na mbichi zilizopatikana mfukoni mwake
B. Ili kumaizi chimbuko na asili ya mihadarati iliyopatikana mfukoni mwake
C. Ili waweze kujionea jinsi dawa za kilevya zilivyokuwa
D. Ili wachunguze iwapo kulikuwa na mwalimu yeyote aliyehusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya
8. Walimu walikenua midomo. Hii ilikuwa ishara ya
A. Kukasirika
B. Kufurahi
C. Kushangaa
D. Kuridhika
9. Kilichomfanya Matata ashiriki katika biashara hii haramu ni
A. Urafiki na wendani walanguzi wa mihadarati
B. Tamaa ya pesa
C. Malezi mbaya
D. Kutomamkinika kwa walimu
10. Anwani ifaayo makala haya si
A. Siku za mwizi ni arubaini
B. Utumizi wa dawa za kulevya
C. Jukumu la walimu katika kukabiliana na mihadarati
D. Wakazi wa Mashaka wajutia vitendo vya Matata

1.1. Kifungu cha Kujibu Maswali Sehemu ya Kwanza - Majibu [you need to sign in first and to sign in, you must be a member]

1.0. Kifungu cha Kujibu Maswali Sehemu Nunge - Maswali

1.2. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Kwanza Sehemu ya Pili - Maswali

fasihi