2.0. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:25 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-13


Maradhi ya moyo yamekuwa yakiwaathiri watu wengi hasa kutoka kubadilika kutokana na kubadilika kwa hali ya maisha .Lakini watafiti wamebaini wagonjwa wanaochukua muda kutafakari hupunguza hatari ya kufariki kutokana na maradhi ya moyo.Utafiti uliofanywa na chuo cha matibabu cha wiscosin kwa ushirikiano na chuo kikuu cha maharishi lowa na yaliyotolewa wakati wa mkutano wa cha ma cha mayo Amerikani .
Walichunguza wagonjwa 201 ,waamerika –weusi kwa kuwafanya baadhi kutafakari na wengine wakapewa mafunzo ya kubadilisha mitindo ya maisha .Baada ya muda wa miaka tisa ,waligundua kuwa waliotafakari walipunguza hatari ya kufariki kutikana na mshtuko wa moyo au kufyunza ganzi kawa asilimia 47 .Waliochunguzwa walikuwa na umri wa kadiri miaka 59 na walikuwa na mishipa ya moyo iliyokuwa miembamba .
Kundi la kutafakari lililulizwa lifanye hivyo kwa dakika 20 kila siku .Kundi la kubadili mtindi wa maisha lililpokea mafunzo ya kawaida kuhusu hatari za kawaida ,kubadilisha lishe na mazoezi .Baada ya miaka tisa ,kulikuwa na visa 20 (mishtuko ya moyo ,kufa ganzi na vifo )katika kundi la kutafakari na 31 kwa kundi la kubadilisha mtindo wa maisha “Kufikia mwisho wa miaka tisa ,asilimia 80 waliotafakari walikuwa bado wanafanya mazoezi zaidi ya mara moja kwa siku . Lakini kulikuwa na mabadiliko haba sana katika kundi lililopokea mafunzo ya kiafya ,”alisema Dkt.Robert Schneider, aliyeongoza utafiti.
1. Maradhi ya moyo __________
A. Yamekuwa yakiwaadhiri watu wengi
B. Hayapo tena
C. Ni ya kutisha sana
D. Ni ya manufaa
2. Kwa nini maradhi haya yamewaathiri watu wengi ?
A. Bure tu
B. Kutokula vibaya
C. Kutokana na kubadilika kwa hali ya maisha
D. Uongo tu
3. Neno wamebaini limetumika katika ufahamu .Lina maana gani ?
A. Wamgundua
B. Wamejuta
C. Wamezungumza
D. Wameleta
4. Watafiti wamebaini kuwa ________________
A. Ugonjwa wa moyo ni mbaya
B. Pia kuna ukimwi
C. Wagonjwa wanaochukua muda kutafakari kupunguza hatari ya kufariki kutokana na maradhi hayo
D. Wagonjwa wapo
5. Utafiti ni nini ?
A. Usayansi
B. Kuchokora
C. Kusema ukweli
D. Kuchunguza ukweli
6. Utafiti ulifanywa na chuo cha matibabu cha Wisconsin kwa ushirkiano na chuo kikuu cha maharishi. Ushirikiano ni sawa na ?
A. Kukubaliana
B. Wakiungana
C. Wakizungumza
D. Wakiogopa
7. wachunguzi walifanya utafiti kwa watu 201 na wengine wakafanyiwa nini ?
A. Wakapewa afunzo ya kubadilisha mitindo ya maisha
B. Wakachunguzwa zaidi
C. Wakaambiwa wanywe dawa za moyo
D. Wakaachwa hivyo
8. Lengo la kuwapa ushauri lilikuwa _______
A. Kupunguza pesa za utafiti
B. Kuwapora pesa
C. Kupunguza hatari za kufariki
D. Kuua watu
9. waliochunguzwa ___________
A. Wakiendelea kuaga dunia
B. Wakiwa wagonjwa zaidi
C. Bure tu
D. Walikuwa na umri wa kadri wa miaka 59
10. watu hawa waliokuwa na umri wa kadri miaka 59 walikuwa na nini ?
A. Wazee
B. Wagonjwa sana
C. Ni mishipa ya moyo iliyokuwa miembamba
D. Mchezo sana
11. kundi la kubadili mtindo wa maisha lililpokea nini ?
A. Mafunzo ya kawaida kuhusu hatari za kawaida ,kubadilisha lishe na mazoezi
B. Pesa nyingi zisizo za kawaida
C. Hongo kubwa sana
D. Bidhaa nyingi za utafiti
12. Baada ya miaka ishirini baada ya kupewa mafunzo
A. Kulikuwa na visa 201 vya mshtuko wa moyo na kufa ganzi na vifo
B. Kulikuwa na vifo vingi
C. Kulikuwa na visa 20 vya mshtuko wa moyo ,kufa ganzi na vifo
D. Maisha magumu
13. kichwa kifaacho ufahamu huu ni kipi ?
A. Utafiti husaidia kuimarisha moyo
B. Ugonjwa wa moyo
C. Moya mkuu
D. Utafiti
fasihi