2.2. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 4:30 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-12


Kwa mara nyingine ,mtandao umekuwa kivutio kwa wanaotaka kusababisha wengine kero.Sasa ,wote na anwani ya barua pepe ya hotmail wamepokea ujumbe unaosema imeishiwa na nafasi ya akaunti zao.”Mtumiaji,kutokana na idadi kubwa ya ghafla ya watu wanaofungua akaunti mpya ya hot mail ,tumegundua kwamba rasilmali zetu za nafasi zinatokomea .Kwa hivyo ,katika kipindi cha mwezi mmoja, yeyote ambaye hatakuwa amepokea barua pepe hii ikiwa na anwani yake ilivyo ,atakuwa amefutwa kutoka kwa orodha yetu ya wateja .
Tunataka tujue ni kina nani ambao wanatumia akaunti za hotmail ,kwa hivyi ikiwa unatumia ,tafadhali msukumie mteja mwingine ujumbe huu mara moja .Na ikiwa hutausambaza ,tutakufuta katika orodha ya wateja wetu.”Hata hivyo ,wamiliki wa hotmail wamekanusha ujumbe .Isitoshe ,imetambuliwa kuwa ni mojawapo ya hila ambazo zimekuwa zikisambazwa tangu 1999.Hila hizi zinapatikana kwa simu na mtandao mwingine .
“Hata kama hotmail inaishiwa na rasilmali ,bila shaka itatumia mbinu nyingine ya kuwasiliana na wateja wake,badala ya kuwaambia wasambazie wenzao ,”Hotmail inasema imekuwa kawida kwenye wenye kutumia mbinu sawa na hili kunasa habari za kibinafsi za watu na hatimaye ………………..
1. Mtandao imekuwa kivutio kwa kina nani?
A. Kila mtu
B. Watu wakubwa pekee
C. Kwa wale wanaotaka kusababishia wengine kero
D. Wale wameutamani
2. neno kero limetumika katika ufahamu .lina maana sawa na__________
A. Kufuraisha watu
B. Kuudhi watu
C. Kusingizia watu
D. Kuimarisha watu
3. wote walio na anwani ya barua pepe wamepokea ujumbe unaosema ______
A. Imeishiwa na nafasi ya akaunti
B. Wasitumie mtambo huo tena
C. Kenya inazoroteka
D. Akaunti inaharibika
4. Kulingana na ufahamu _____
A. Watu wengi hawapendi mtandao
B. Hakuna mtandao wa hotmail
C. Kuna idadi kubwa ya ghafla ya watu wanaofungua akaunti mpya za hotmail
D. Vijana ndio wanaofungua hotmail
5. Nini ambazo zinatokomea ?
A. Akaunti
B. Wateja wa hotmail
C. Rasilmali zetu za nafasi
D. Stima
6. Yeyote atakayepata barua pepe ikiwa na anwani yake ilivyo,________
A. Atakuwa amefutwa kutoka kwa orodha ya wateja
B. Atakuwa hajafutwa kwa orodha
C. Hamna jambo litamtendekea
D. Atakuwa salama
7. Ikiwa mtu anatumia akaunti ya hotmail kasha apate berua pepe hiyo ,_______
A. Asiwe na shaka
B. Awe na shaka
C. Aachane na akaunti ya hotmail
D. Amsukumie mteja mwingine ujumbe huu mara moja
8. Tishio analotolewa mtu ambaye hatasambaza ujumbe huu ni lipi?
A. Kufutwa katika orodha ya wateja wa mtandao
B. Kuendelea kuwa mteja wa mtandao
C. Kutokuwa na uwezo wa kusoma barua pepe
D. Kuwa na uwezo wa kufutwa katika mtandao
9. Watumizi wa hotmail __________
A. Wametoroka hotmail
B. Wamekanusha ujumbe
C. Hawapendelei hotmail tena
D. Ni wabaya
10. Kama hila zimekuwa zikitangazwa kutoka wakati uliotajwa ,na tuko mwaka wa 2009 ,ni miaka ngapi ambayo imepita sasa?
A. Kumi
B. Ishirini na tatu
C. Saba
D. Karne
11. Hata kama hotmail inaishiwa na rasilmali _________
A. Yafaa iendelee kutafuta wateja
B. Haina bahati hata kamwe
C. Yafaa itumie mbinu zingine za kuwasiliana na wateja wao
D. Iendele kusambaza ujumbe kivyao
12. Kichwa kifaacho cha ufahamu huu ni kipi ?
A. Mtandao
B. Wasambaza ujumbe juu ya kituo ‘hotmail’
C. Hotmail
D. Barua pepe
fasihi