2.5. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Tano - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 11:10 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Hatua ya serikali ya Uingereza kuwalipa fidia wakenya walioteswa na serikaliya wakoloni ilipokabiliana na wapiganaji wa Maumau haifai kushangiliwa jinsi baadhi ya watu wanavyofanya. Inasikitisha kwamba baadhi ya watu wanasifu hatua hiyo bila kuzingatia masaibu waliopitia wapiganiaji hao ambayo yanawaandama hadi wakati huu.
Kitita cha shilingi bilioni mbili nukta sita ambacho serikali hiyo ilitoa kwa wapiganaji elfu tano walioshtaki Uingereza kupitia kwa tume ya hakiza kibinadamu ya Kenya ni kama dharau kwa wapiganiaji hao. Watakaonufaika na fidia hiyo ni walionusurika kifo wakati wenzao waliuawa. Ni wale waliotumbukizwa vizuizini wakahasiwa na makovu ya dhuluma hizo yatadumu milele. Dhuluma zilikuwa za kinyama kiasi kwamba hakuna kiwango cha pesa kinachowezakuzifidia. Kwamba serikali ya Uingereza iliamua kusulusisha kesi hiyo nje ya mahakama ni ishara kwamba ilikuwana hakika kwamba mahakama ingewapa wapiganiaji hao fidia kubwa.
Maovu ambayo wapiganiaji wa Mau Mau walipitia kwa ajili ya nchi hii ni mengi. Kweli walikata pua ili waunge wajihi . serikali inastahili kuwatambuana kuhakikisha kwamba baadhi yoa wakilala bila chakula na kuishi katika mabanda sawa na iliyokuwa walipopambana na wakoloni kukomboa nchi hii ambayo wanasiasa wanafurahia. Katika mila za kiafrika , ni laana kumpuuza mtu aliyemwaga damukwa ajili yako na kutowajali wapiganiaji hao huenda kumesababisha hali ilivyo katika nchi hii ambapo maovu yanazidi kukolea huku maadili yakiendelea kumomonyoka.
Wazee walioingia msituni kupigania nchi hii na akina mama walioteswa wakidaiwa kuhusika na wapiganiaji hao wanastahili fidia ya kutosha. Serikali ya Uingereza iliwachezea shere wapiganiaji hao kama ilivyozoea kufanya katika mambo mengi. Kumbuka Uingereza ingali katika dhana potovu kuwa mwafrika hawezi kujiamulia shida zake. Wakae wakijua kuwa mjinga akierevuka mwerevu yu mashakani.
Hata hivyo ifahamike kuwa , kwa kusema haya siwachochei wapiganiaji hao kukataa pesa hizo zilizotolewa, ila ninashawishika kwadhati kuwa mengi yalihitajika kufanywa. Badala ya kukimbilia hela chache kama hizo, ingekuwa bora kama Uingereza ingeanzisha wakfu maalum wa kuwatunza Wamaumau hao, kuwasomesha wana wao, kuwajengea makao na kuhakikisha wanaishi maisha mema. Kwa kuanzisha wakfu huo na kutegemea pesa za kushughulikia kila mwaka, kungewafaidi wakongwe haoambao baadhi yao wanaugua vidonda vya moyo visivyopenyeka kwa hela chache bali haki.
Katika suala hili, serikali ya Uingereza ilijitia kitanzi. Sasa sina shaka kwamba, kwa kufidia wapiganiaji hao, Uingereza ilifungua mlango kwa madai kama hayo kutoka pembe zote za dunia ambako watawala wake walitekeleza maovu chini ya ukoloni.

1. Kulingana na aya ya kwanza,______
a. Mwandishi anafuraia hatua ya serikali ya Uingereza kulipa fidia.
b. Wakenya walioteswa na serikali ya mkoloni hawakulipwa chochote.
c. Mwandishi hajafurahia fidia iliyolipwa na serikali ya Uingerezakwa wapiganiaji wa maumau.
d. Serikali ya Uingereza ulizingatia masaibu ambayo Mau Mau walipitia katika kulikomboa Taifa hili.
2. Wapiganiaji wa maumau walitumia njia gani kuwasilisha malalamiko yao?
a. Tume ya katiba na maswala ya haki nchini.
b. Tume ya haki za kibinadamu ya Kenya.
c. Wapiganiaji wa maumau ambao waliuliwa. Tume ya maridhiano na haki za kibinadamu nchini Uingereza.

3. Kulingana na makala haya, kitita cha shilingi bilioni mbili nukta sita___
a. Ni kiasi kidogo sana kikilinganishwa na dhulma walizopitia Wanamaumau.
b. Ni kiasi kikubwa sana cha pesa kwa kuwa si wengi hulipwa kiasi hicho cha pesa.
c. Ni kiasi kikubwa sana cha pesa kikilinganishwa na masaibu ya Wanamaumau.
d. Ni kiasi cha pesa ambacho hakipaswi kupuuzwa na Mkenya mwenye masaibu.
4. Kweli walikata pua ili waunge wajihi. Hii ina maana kuwa____
a. Wakoloni wengi waliwanyanyasa wakenya kwa kuzikata pua zao.
b. Wanamaumau walishiriki katika vita ambavyo ingawa viliwahasiri vilililetea taifa hili manufaa ya uhuru.
c. Wanamaumau waliamua kuzikata pua zao ili kuonyesha kero kwa serikali ya mkloloni
d. Sura za wakenya wengi zilikuwa mbaya hususan kwa kuwa na pua ndefu
5. Kwa maoni mwandishi, maadili yanazidi kumomonyoka_____
a. Baada ya vijana kupuuza mawazo ya wakubwa wao.
b. Kwa kuwa siku hizi walimu na wazazi wamekwepa majukumu yao ya ulezi.
c. Kwa sababu ya mashindano makali baina ya jinsia ya kike na ile ya kiume.
d. Kwa kupuuza mchango wa wale waliomwaga damu na kuupigania uhuru wa wakenya.
6. Fidia ni malipo yapi?
a. Yanayolipwa mtu baada ya kuhusika katika ajali
b. Malipo kwa ajili ya hasara
c. Ni yale yanayolipwa aliyechafuliwa sifa.
d. Ya kuingia vitani.
7. Katika mwanzo wa aya ya nne, neno ‘wazee’ limetumika kwa maana ya____
a. Wote walioingia msituni kupigana na serikali mkoloni.
b. Wanaume na wanawake waliokula chumvi nyingi.
c. Wanaume waliobugia chumvi nyingi.
d. Wote waliochangia kupigana na serikali ya mkoloni.
8. Ni nini maana ya ‘kuchezea shere’ ?
a. Kunyanyasa
b. Kudhulumu
c. Kuhadaa
d. kupendelea
9. kwa maoni ya mwandishi, suluhisho la kudumu lingekuwa:-
a. kuongeza kiasi cha pesa ili ziwezekukidhi mahitaji ya kila Mwanamaumau
b. kuanzisha wakfu wa kuwafaa Wanamaumau wakati wa taabu.
c. Kuhakikisha kuwa serikali ya Uingereza imeomba msamaha kwa dhulma ilizofanyia Wanamaumau.
d. Kukata kuchukua pesa zozote kutoka kwa serikali ya Uingereza.
10. Kauli inayosimamia makala haya ni kuwa____
a. Fidia ni bora lakini wakfu ni bora zaidi.
b. Fidia ni bora kuliko wakfu.
c. Wakfu ni bora kwa kuwa hauhitaji pesa zozote.
d. Fidia ni bora sawa wakfu lakini fidia ni bora zaidi.
kiswahili revision papers