2.6. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Sita - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 20, 2015, 11:20 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Kijana Matata alizaliwa katika kijiji cha Mashaka mwaka wa elfu moja kenda mia tisini na tatu. Kama ilivyo kawaida katika mila na desturi za Waafrika, mwana ni tunu kutoka kwa Mola. Wengi wa wanakijiji walifurahia kuingia kwa Matata duniani. Hali hii ilichochewa na idhibati ya wana waliokuwa wamezaliwa hapo awali. Wengi baada ya kupata kisomo waliishia kuwa watatuzwa shida kemkem zilizo wakumba wakazi waq eneo lao. Walitarajia Matata afuate nyayo za watangulizi wake na kuyafanya maisha ya wakazi kuwa rahisi lakini hivyo sivyo mambo yalivyokuwa.
Baada ya Matata kujiunga na shule ya msingi, masomo yake yaliendelea vizuri hadi pale alipofika darasa la saba.alianza kuingiwa na uchuwa wa pesa. Aliamua kuwa akiwasaidia walanguzi wa dawa za kulevya ambao tayari walikuwa wamebadilisha mbinu za kusafirisha dawa hizo. Walanguzi hawa waliamua kumtumia Matata ili kukwepa mkono mrefu wa sheria. Wao walifanya hivi kwa kuwa sio rahisi kwa mafias wa polisi kudadisi au hata kushuku mwanafunzi. Kufuatia hali hii kamishna wa polisi aliwahimiza walimu wakuu wa shule ya msingi na upili kuwa makini na kuwafuatilia mienendo ya wanafunzi wao kila wakati.
Kutokana na utumizi mwingi wa dawa za kulevya, mwalimu mkuu wa shule aliyoisomea Matata aliamua kualika mshaurinasahe ili kuwahutubia wanafunzi. Alianza, “Wanafunzi ambao wako shuleni hivi sasa ndio tegemeo la taifa hili siku zijazo na itakuwa hasara kubwa iwapo watajiingiza katika lindi la matumizi ya dawa za kulevya. Itakuwa sio sawa kwetu kulinyuamazia suala hili, hivyo basi ni wajibu wetu kulivalia njuga na kutumia kila mbinu ili kuokoa maisha ya wanafunzi. Tusipo fanya hivi udongo utakauka na itakuwa vigumu kuuwahi.
Walimu ni lazima muwe makini na mandhari yanayozunguka shule na msisite kupiga ripoti katika kituo chochote cha polisi iwapo mtagundua harakati zozote za biashara hiyo haramu zikiendeshwa. Kumbukeni kunyamaza kwenu kutakuwa sawa na kuchangia katika uovu huo. Dawa za kulevya ukizizoea zinakuwa ni saratani. Athari zake ni nyingi hususan kwa wanafunzi , kwa matokeo yake hudorora katika tamrini za madarasani, utovu wa nidhamu na pia hizi huathiri afya ya mtumiaji. Walio katika uraibu huu wakome mapema kwa kuwa usipoziba ufa utajenga ukuta.”
Matata alikuwa ametega masikio ndi! Kwa kuwa walimu walikuwa wameona yote yaliyosimuliwa na mshaurinasaha kutoka kwa Matata; walimwita ili kumdadisi kiasi. Walishangaa walipotumbukiza mkono kwenye ukoba wa Matata na kupata pakiti kadhaa za dawa za kulevya. Papo hapo walimketisha chini ili kubaini mbivu na mbichi. Hapo Matata aliwafungulia moyo na kuwaeleza walimu wake vile ambavyo amekuwa akitimiwa na walanguzi wa dawa za kulevya. Walimu walikenua mdomo yao wasiweze kuamini kuwa walikuwa wamefeli katika majukumu yao iwapo kwa muda wote huo hawakuwahi kugundua kuwa Matata alikuwa mraibu wa mihadarati. Matata aliamua kubadilika huku akisadiki kuwa mui huwa mwema.

1. Wakazi wa kijiji cha Mashaka, walifurahia kuzaliwa kwa Matata kwa kuwa,___
a. Mototo ni tunu kutoka kwa Mola.
b. Wengi wa wana waliozaliwa hapo awali walichangia katika kutatua shida zao.
c. Matata alikuwa mwana wa kipekee aliyekuwa aakipawa cha pekee.
d. Alionekana kuwa mtatuzi wa shida nyingi zilizowakumba wakazi wa eneo hilo.
2. Kwa nini walanguzi wa mihadarati waliamua kumtumia Matata katika biashara yao?
a. Matata alikuwa amependezwa na kazi hiyo tangu alipozaiwa.
b. Watumizi wengi wa dawa za kulevya walikuwa ni wanafunzi.
c. Lengo lao lilikuwa kukwepa mkono mrefu wa sheria.
d. Matata mwenyewe aliamua kuwa akiwasaidia katika biashara hiyo.
3. Msemo “uzee hula ujana” unajitokeza pale,
a. Wanafunzi waambiwa kuwa hao ndio tegemeo la taifa letu la siku zijazo.
b. Kamishna wa polisi anawataka walimuwakuu wawe waangalifu na mazingira ya shueni.
c. Mwalimu mkuu anamwita mshaurinasaha kuzungumzia suala la mihadarati.
d. Watoto wengi wa mtaa wa Mashaka walinukia kuwa watatuzi wa shida nyingi ya wakazi.
4. Ni nini maana ya “ujumbe uliopigwa kistari?
a. Udongo mgumu haukandikiki kwa uraisi.
b. Wanafunzi wasipotilia maanani bidii shuleni watakuwa wakifanya kazi za udongo.
c. Mwanafunzi anayetumia mihadarati ni sawa na nyumba ya udongo
d. Walimu wakichelewa kukabiliana na tatizo la mihadarati, kizazi kitakuwa kimepotea.
5. Athari za dawa za kulevya kwa mwanafunzi kulingana na makala haya ni ____
a. Kusinzia darasani, kuchoka ovyo na utovu wa nidhamu.
b. Utovu wa nidhamu, kufeli katika mtihani na kuchoka.
c. Kuugua, kufeli mtihani na utovu wa nidhamu.
d. Kuugua, kusinzia darasani na utovu wa nidhamu.
6. Kichocheo kikuu cha mwalimu mkuu kumwalika mshaurinasaha kilikuwa____
a. Yeye hakutaka kulaumiwa na kamishna wa polisi ati alikuwa ameshindwa na kazi yake .
b. Hakuwahi kulizungumzia dawa za kulevya.
c. Aliwashuku baadhi ya wanafunzi kuwa walanguzi wa mihadarati.
d. Utumizi mkubwa wa mihadarati katika eneo husika.
7. Kwa nini walimu walimketisha Matata chini?
a. Ili kubaini dawa mbivu na mbichi zilizopatikana mfukoni mwake.
b. Ili kumaizi chimbuko na asili ya mihadarati iliyopatikana mfukoni mwake.
c. Ili waweze kujionea jinsi dawa za kulevya zilivyokuwa.
d. Ili wachunguze iwapo kulikuwa na mwalimu yoyote aliyehusika na ulanguzi wa dawa za kulevya.
8. Walimu walikenua midomo. Hii ilikuwa ishara ya____
a. Kukasirika
b. Kufurahi
c. Kushangaa
d. kuridhika
9. kilichomfanya Matata ashiriki katika biashara hii haramu ni____
a. urafiki na wendani walanguzi wa mihadarati
b. tama ya pesa
c. ma lezi mbaya
d. kutomakinika kwa wlimu
10. Anwani ifaayo makala haya si____
a. Siku za mwizi ni arubaini.
b. Utumizi za dawa za kulevya.
c. Jukumu la walimu katika kukabiliana na mihadarati.
d. Wakazi wa Mashaka wajutia vitendo vya Matata.

kiswahili revision papers