2.7. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Saba - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 21, 2015, 9:59 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Kuzinduliwa kwa elimu bila malipo ilikuwa ni zawadi iliyotunukiwa wakenya na serikali ya NARC punde tu baada ya kushika hatamu za uongozi. Mpango huu ulianza kutekelezwa mnamo Januari 2003 . serikali ilifanikisha kwa kuutengea kitita cha shilingi bilioni tano nukta sita katika bajeti yake. Kila shule hugawiwa pesa hizi kulingana na idadi yake ya wanfunzi. Pesa zenyewe hufika shule moja kwa moja kutoka kwa serikali kupitia akaunti ya shule katika benki.
Elimu hii ilipoanziwa, idadi ya wanafunzi wanojiunga na shule iliongezeka kwa zaidi ya wanafunzi limesababisha changamoto kwa walimu kubuni mbinu mpya za kufunza ili kukabiliana na msongamano wa wanafunzi darasani . Aidha ,walimu wamejikuta wakipambana na wanafunzi wenye umri uliotofautiana. Wengine wakiwa wamekula chumvi nyingi ilhali wengine niwa umri wa chini.
Miongoni mwa wanafunzi wenye umri mkubwa waliojiunga na elimu hii ilipozinduliwa ni mzee mwenye umri wa zaidi ya miaka themanini! Mzee huyu anaitwa Kimani na alijiunga na shule moja huko Eldoret katika darasa la kwanza.
Kwakweli hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Ukosefu wa kutosha nitatizo linguine lililoukumba mpango huu mwanzoni. Hii ilitoka na serikali kuhusu uajiri wa walimu ya kuajiri kiasi kidogo tu kati ya wale wanaofuzu vyuoni.
Ukosefu wa vifaa vya kutosha, kama vile madawati , pia kikwazo kingine . Katika baadhi ya shule vijijini si nadra kuwaona wanafunzi wakisoma wakiwa wameketi sakafuni.
Ubora wa elimu itolewayo huenda uliadhiriwa kidogo na matatizo hayo. Palionekana kuzuka tofauti kubwa katika matokeo ya mtihani wa K.C.P.Ebaina ya shule za umma na zile za kibinafsi.
Mgala muue na haki umpe. E4limu bila molipo imepiga hatua kubamba katika kutimiza lengo la serikali la elimu kwa wote na kufanya Kenya iwe na watu wengi wanaojua kusoma na kuandika. Piaimesaidia kutimiza haki ya elimu kwa watoto.
Vifaa muhimu kama vitabu vimekuwa vikitolewa na hili limewavua wazazi mzigo mkubwa. Imekuwapia furaha na buraha kwa wanafunzi maadamu huweza kuhudhuria masomo kila siku bila hofu ya kufukuzwa wakalete karo.

1. Serikali ya NARC iliwafanyia nini wananchi wake.
a. Mshahara mnono
b. Kuleta vyama vingi
c. Elimu ya bure
d. Ongezeko la watoto
2. Kisawe cha kushika hatamu ni
a. Kushika mkia
b. Kushika mguuni
c. Kushika tama
d. Kushika usukani
3. Mambo yana yihitajikana ili shule ingawiwe pesa ni
a. Idadi ya wanafunzi na madarasa
b. Idadi ya wanafunzi na akaunti ya benki
c. Akaunti yake ya benki
d. Idadi ya wanafunzi na walimu
4. Kuzinduliwa limepigwa mstari lina maana ya
a. Kuanishwa
b. Kuamshwa
c. Vumbua
d. kuamshwa
5. idadi ya wanafunzi shuleni imesababishwa____kwa walimu
a. nafuu
b. tisho
c. tatizo
d. makabiliano
6. Nilipi ambalo si tatizo katila elimu bila malipo
a. Walimu
b. Vitabu
c. Madawati
d. Madarasa
7. Umri wa mzee Kimani alipojiunga na masomo ni
a. Karne
b. Mwongo moja
c. Korija
d. Zaidi ya themanini
8. Aliyekula chumvi nyingi ni
a. Shaibu
b. Makamo
c. Barobaro
d. kigoli
9. Methali mgala muuwe na haki umpe ina maanisha
a. Usipumbazwe tu na uzuri , ona pia kasoro
b. Ni haki ya kila motto kupata elimu
c. Usione tu matatizo ya jambo ona pia uzuri wake
d. Elimu ya bure ina manufaa mengi
10. Kichwa kifaacho kifungu hiki ni
a. Elimu ya NARC
b. Elimu ya bure
c. Elimu ya ngumbaru
d. Serikali ya NARC

kiswahili revision papers