2.8. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Nane - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 24, 2015, 11:23 PM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Kuliondokea kijana mmoja ambaye mungu alimtunukia ubongo .kijana huyu alijiulikana kama Makame .Darasani alikuwa hawezekani .Akasoma kwa bidii hadi akafika chuo kikuu na kuvunja rekodi .Baadaye akaowa mke kufu na kuwapaya watoto ambao nao vilevile walifuata nyayo za wazazi wao .
Jambo lililokuwa linaikera ya akina Makame lilikuwa ni ukosefu wa kuwajibika kwa ndugu. kaka zake walikuwa wazembe , kila walipohimizwa kama ndugu yao Makame walipuuza na kucheka, walishindwa hata kuchungulia vile vidato vya sekondari vifunguavyo macho na akili zaidi.Tabia zao zikazoroteka wakawa ni walevi wa kupindukia.
Wazazi walipokaribia kuaga dunia ,waliwaita pamoja na kutoa wasia na hata kuwapa urithi wao .Mamake akawambia ndugu zake kuwa kwa vile wao hawana chochote yeye amewapa mashamba ili wayalime na kuweza kujiinua .Wazee walifurahi kuona kuwa Makame alijali majukumu ya wadogo zake .Baada ya vifo vya wazazi hao,wadogo hao hawakuchelewa upiga mali shoka mara moja mamake aliwaonya lakini aliambulia nunge .
Siku moja ajali mbaya ya barabara ikaamua kuyakayisha maiosha mema ya mMakame na mkewe. Huzuni iliwakumbatiwnao lakini majirani na marafiki wakaingilia shughuli za mazishi na kuzimaliza. Watoto walifadhiliwa na majirani hadi wakamaliza shule ya msingi .Nduguze walidhani wamepata vya bwerere na kujiona waklifaidi mali ya Makame na ile ya wazazi wao .Hata hivyo ,juhudi si pato walyoyataka hayakuwa .

1. Makame alidhibitisha werevu wake kwa ___
a. Kupita mitihani
b. Kupita mitihani yote ,kupenda majirani, kuachia wamawe urithi
c. Kuonya ndugu zake
d. Kupenda ndagu zake
2. Wazazi wa makame walikuwa na busara kwani __
a. Waliwapa wana wao wasia
b. Waliwapa wana wao urithi
c. Walikuwa na maonyo mengi
d. Waliwaonya wana wao wakasikia
3. Ndugu za Makame waliposhauriwa wasome walicheka kwa sababu ___
a. Hawakuona haja ya kusoma
b. Walishindwa kuendelea kusoma
c. Makame hakuwa tajiri ijapokuwa alisoma
d. Walitarajia kufaidi mali ya ndugu yao
4. Nduguze Makame ___
a. Walisoma gumbaru wakakosa kazi
b. Walifundishwa kazi ya jua kali wakashindwa
c. Walisomea kazi zas ufundi
d. Waliachia masomo shule za msingi
5. Maana ya mke kufu yake ni
a. Mke wa jamii yake
b. Mke aliyelingana naye
c. Mke wa kijiji chake
d. Mke aliyesoma naye
6. Baada ya kifo cha wazazi wake Makame ,nduguze ___
a. Walidhani watafaidi mali
b. Waligawiwa mali wengine wakafuja
c. Walianza kufuja mali mara moja
d. Walimnyima makame urithi wote
7. Haki za watoto zilitimizwa kwa_____
a. Kutoruhusu watu kuwadhulumu
b. Kusomeshwa,kusaidiwa walipofiwa,kupewa urithi wao
c. Kunyimwa urithi wao
d. Kusomeshwa ,kuonywa na kusaidiwa
8. Kupiga mali shoka ni ____
a. Kutumia mali vibaya
b. Kugawanya mali yote
c. Kuhifadhi mali yote
d. Kupiga mali bei
9. Methali inayofaa pale majirani na marafiki walipowasaidia wale watoto ni_____
a. Damu ni nzito kuliko maji
b. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
c. Ndugu mvi heri naye
d. Kenda ni bora kuliko kumi nenda rudi
10. Ni nini maana ya neon hakikuwasitiri?
a. Hakikuwafunikia aibu
b. Hakikuwakamilisha
c. Hakikuwatamanisha
d. hakikuwatosheleza

kiswahili revision papers