2.9. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Pili Sehemu ya Tisa - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 23, 2015, 11:43 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Uzalendo ni hali ya kuipenda nchi yako kwa moyo wa dhati .Mara nyingi viongozi wetu huhimiza vijana kuwa na uzalendo .Swali ambalo lafaa tujiulize ni hili.Uzalendo huanzia wapi ?Uzalendo lazima nyumbani.Kijana ama mtu yeyote ahakikishe kwamba anapenda nyumbani kwao .Kupenda nyumbani ni sawa na sawa na kupenda wazazi wako na kusikia maagizo unayopewa naoi mara kwa mara .Kijana sharti awe na nidhamu ikianzia nyumbani vijana wetu bila shaka watakuwa na nidhamu shuleni .Wakufunzi wao hawatakua na matatizo yoyote ya kuwafunza vijana hawa .Vijana wetu waliitikaia maagizo na masharti wanayopewa na wakubwa wao basi migogoro shuleni , vyuoni na hata kazini haitakuweko .
Kijana hawezi kuwa rraia mwema ikiwa anadharau utamaduni wake .kila kijana akumbuke kuwa mwacha mila ni mtumwa .Mila zetu ,desturi zetu,madhehebu yetu na imani zetu ndiyo nguzo ya raia mwema ambaye atashiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa .kupenda utamaduni wa nchi yako ndio uzalendo tunaozungumzia .vijana wetu ndio wa leo ndio viongozi wetu wa kesho .Endapo hawaa hawataongozwa vyema na wazazi pamoja na jumuiya wanamokal;ia ,basi nchi yetu itakuwa na viongozi wa kusaliti nchi yao.Uzalendo ndio silaha pekee ya kuimarisha nchi yetu kisiasa , kitamaduni na kiuchumi .
Maovu yote yanayotukabili yataondolewa ikiwa vijana wetu watazingatia uzalendo wan chi yao . Ndiposa rais wetu huwa anatuusia kuwa yeyote anaye jiingiza katika vitendo vya kluhujumu nchi yake ,si mkenya halisi .Mkenya lazima apinge siasa ya kubomoa nchi yake .falsafa ya mtu ya mtu kama huyo lazima iambatane na msaingi ya kidemokrasia iliyokubaliwa na wote .Nchi yetu ni kama mama yake .mtu kama huyu huwa hana uzalendo wowote wan chi yake .vijana wetu wajitoe mhanga kwa jino na kucha kupigania amani ,upendo na umoja katika nchi yao .
Maovu mengine kama ufisadi ,ukabila,uhasama,magendo pamoja na ulanguzi yataondolewa miongoni mwetu ikiwa tutazingatia swala la uzalendo .watu wana moyo wa tama ni kitu kibaya na wakati mwingine huzaabana . kuna watu ambao wanataka kujitayarisha kwa haraka bila kujali matakwa ya taifa .watu kama hawa ni nadra sana kuzingatia maswala ya kitaifa .
Ubinafsi unaowatawala na aghalabu huwa na wamefunikwa na wingu jeusi wasione mbele . utamwona mtu kama huyu akiwa mbadhirifu wa fedha kwa kuwanun ulia watu pombe huku hafikirii kutoa chochote mikutano ya harambee.muungwana ni kitendo ,hivya ndivyo walivyosema ,wahenga wetu .
Ikiwa watu matajiri hawataweza kusaidia au kuwajali wengine ambao hawakubahatika miongoni mwetu basi matajiri kama hao hawana imani kwa nchi yao .moyo wa kusaidia lazima uwepo . mchango wako kwa maendeleo waweza kuthaminiwa ikiwa uliotoa kwa moyo mkunjufu ,kwani kutoa ni moyo usambe ni utajiri .sisi sote tuwe na nidhamu kazini .Tusijiingize katika vitendo vya kuiba serikali saa za kazi kwa malengo yetu sisi wenyewe . Uzalendo ndio nguzo ya taifa lililo9 changa kama letu.

1. Kwa nini mwandishi asema kuwa uzalendo lazima uanze nyumbani ?
a. Kwa sababu wazazi ndio wanaotimiza uzalendo kamili nchini
b. Kutimiza uzalendo nyumbani kunawafanya kuwa na nidhamu wanaieneza shuleni na nchi nzima
c. Wazazi huwa na saa nyingi za kuwafunza vijana uzalendo
d. Lugha ya mama kutumiwa vizuri kuhimiza uzalendo
2. Nidhamu ni nini kulingana na muktatha wa kifungu hiki ?
a. Mizizi ya maisha bora nchini
b. Chanzo cha uzalendo nchini
c. Chanzo cha mapenzi nyumbani
d. Hatua za kuondoa migogoro nyumbani.
3. Mwandishi ametumia neno’[utamaduni’ kuwasilisha nini?
a. Hali ya maisha siku za usoni
b. Imani ya desturi na mila zetu za kiafrika ambazo ndizo nguzo za raia mwema
c. Mila na desturi za kiafrika
d. Kudharau mila na desturi ni kigeni
4. Ni jambo lipi la muhimu linaloweza kumaliza migogoro shuleni?
a. Vijana kuwapenda walimu na wazazi wao
b. Vijana kutiwa adabu na walimu wao
c. Vijana kuitikia maagizo na masharti wanayopewa na wakubwa wao
d. Kijana kushirikiana na wazazi ,walimu na wanafunzi wenzao katika kila jambo
5. Kutokana na maoni ya rais wetu_____-
a. Mtu ambaye ni msaliti wan chi yake si mzalendo
b. Mtu ambaye ana vitendo vya kuhujumu nchi yetu si mkenya halisi
c. Mkenya lazima ajiingize katika siasa ya kutunza nchi na kuwasaliti wenzake
d. Vijana wetu wachukue silaha kupingania haki
6. Kwa nini uzalendo umelinganishwa na silaha ?
a. Kwa sababu mzalendo anaweza kutumia silaha kupigania amani upendo na umoja
b. Ndio ngao ya kuunda amani upendo na umoja wa n chi
c. Nchi ambazo zina silaha nyingi huwa na uzalendo wa kusifiwa
d. Asiyependa amani hutumia silaha kuvunjas amani
7. Migogoro shuleni husababishwa na nini?
a. Karo ya shule kuongezeka
b. Wanafunzi kuongezeka shuleni
c. Walimu na wazazi kutozingatia uzalendo
d. Watoto kutofurahishwa na matendo ya walimu au viongozi wa shule
8. Vijana wanaweza kushiriki vipi katika ujenzi wa taifa ?
a. Kuwa na nidhamu ,kutoendeleza ufisadi ,magendo pamoja na ulanguzi nchini
b. Kuwaajiri vijana wengine kutoka nchi jirani
c. Kuhudhuria mikutano ya kisiasa na kukomesha fujo
d. Kuwakemea walio na elimu ya juu na kutotumia mmawaidha ya wazazi
9. Ni nini hasa kinasababisha ufisadi ?
a. Nchi kuwa na pesa nyingi zilizo na matumizi
b. Wananchi kutowaamini maafisa wa serikali
c. Tama ya kuwa matajiri haraka
d. Ukosefu wa fedha nchini
10. Mwandishi angetumia neon gani badala ya aghalabu?
a. Mara nyingi
b. Imani
c. Nadra
d. agiza

kiswahili revision papers