3.0. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Nunge - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 12:04 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Fatuma alikiona kilichomfanya kuku kukosa meno hivi juzi. Huku michirizi ya machozi ikimchirizika , na akiwa na uchungu mwingi alisikika kwa kusema ,”Ole wangu majuto ni mjukuu, kama ningali jua nisingali toa mimba hiyo.sasa nimebaki kaburi mwilini. Mungu wangu naomba unisamehe kwa kuua kiumbe chako bila sababu yoyote.
Fatuma, msichana wa miaka kumi na mine alipata mimba hiyo akiwa kidato cha nne. Alienda kwa mganga wa kichochoroni na mganga huyo alipokuwa akitoa mimba hiyo, fatuma alianza kuvuja damu nyingi hadi akazirai. Mganga kuona mambo yalivyokuwa yakizidi kuwa mabaya alimwacha hapo kitandani na kuitimua mbio .kwa bahati nzuri msamaria mwema alimchukua msichana huyo hadi kituo cha matibabu alikolazwa huko kwa muda wamiezi mitatu.
Jambo la kuhuzunisha no lililomtia Fatuma hofu sana nikujua kuwa alikuwa ameyaangamiza maisha ya kiumbe cha Mungu. Mawazo hayo angali yanamtatiza mpaka leo na kila anapokumbuka kitendo hicho machozi humtoka . Isitoshe daktari pia alimfahamisha kuwa maisha yake ya baadaye, hataweza kuzaa tena kwa sababu sehemu zake za uzazi hasa nyumba ya mtoto ilikuwa imeharibika kabisa.
Uharibifu huo ulikuwa umesababishwa na vifaa ambayo mganga huyo bandia alikuwa kwa utoaji mimba.

1. Nini maana ya michirizi ya machozi?
a. Machozi yalimlenga machoni
b. Machozi yalimjaa machoni
c. Kulia bila kutoa sauti ya kwikwi
d. Njia nyembamba ya machozi
2. Maana ya methali “majuto ni mjukuu” ni
a. Majuto ni motto wa mwanawe babu
b. Utajua ukichokoza mwenzako
c. Ukifanya matendo mabaya au kukosa utajuta baadaye
d. Ukienda kwa mwendo wa kufanya jambo kwa wakati wake,utasikitika polepole
3. Fatuma alijiunga na shule ya upili akiwa na umri wa miaka
a. Kumi na mitano
b. Miaka kumi na sita
c. Miaka kumi na minane
d. Miaka kumi na minne
4. Kulingana na habari hii,baada ya kutoa mimba Fatuma alithibitishwa kuwa
a. Muuaji
b. Tasa
c. Mganga
d. kahaba
5. kwa nini mganga alitimua mbio?
a. Kwa sababu fatuma alikuwa amefariki
b. Kwa sababu aliogopa damu nyingi iliyoendelea kuvuja
c. Kwa sababu alikuwa ameangamiza kiumbe cha Mungu
d. Kwa sababu alikuwa na hofu fatuma alipotokwa na damu nyingi kasha akazirai
6. Ni mawazo yapi ambayo yangali yanamtatiza fatuma mpaka leo?
a. Kuangamisha kiumbe cha mwenyezi Mungu
b. Fikira kwamba hatazaa tena
c. Kuharibiwa maisha na mpenziwe Hamisi
d. Kutokwa na damu nyingi
7. Ni msemi ipi ufaao kutumiwa badala ya”kutimua mbio”
a. Kwenda kukuru kakara
b. Kwenda shoti
c. Kutimua timutimu
d. Kwenda pukutu!pu
8. Maana ya neno kuzirai ni
a. Kufariki
b. Kupotewa na fahamu
c. Kushikwa na kizuzi
d. kulala
9. Neno jingine sawa na ‘kutoa mimba’ni
a. kuavya
b. tasa
c. kuua
d. kunyonga
10. Nyumba ya mototo ni
a. Nyumba anamolala mototo
b. Chupa
c. Mahali ambapo motto hupitia anapozaliwa
d. Mahali mtoto anaishi akishazaliwa

kiswahili revision papers