3.1. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Kwanza - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 12:28 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Watu kumi na saba walifariki dunia katika ajali tofauti katika jimbo la Nakuru,Kiambu na Garissa. Jambo hilo lilijumlisha waliokufa katika ajali za barabara mwaka huo kufika mia nne na themanini na kenda.
Katika ajali ya Nakuru watu wanane walifariki na watu wakajeruhiwa vibaya wakati lori la kubebea ngano lilipoacha barabara na kugonga mkahawa uliojaa watu karibu na kituo cha kibiashara Tandu.Watu sita walifariki papo hapo ilhali hao wengine walifia hospitalini kuu ya mkoa ,Nakuru.
Polisi walisema ajali hiyo ilitokea mnamo saa kumi na mbili jioni jumamosi. Walishuku breki za lori zilikoza kushika ndipo likaacha barabara.Miongoni mwa waliojeruhiwa alikuwa motto wa miwka minane ambaye alivunjika miguu.
Katika ajali ya Kiambu, abiria watatu walifariki dunia hapo papo. Mtu wa nne alifariki alipokuwa akitibiwa katika hosipotali kuu ya wilaya mjini Kiambu. Basi hilo lilikuwa limbeba abiria ishirini na wawili. Polisi walisema mmoja wa waliouliwa na basi alikuwa mama mjamzito.
Katika wilaya ya Garissa lori la serikali liligonana na gari lenye nambari za Somalia na watu watano wakaaga.
1. Kutokana na taarifa hii,ni wilaya ngapi zilizotajwa
a. Sita
b. Tatu
c. Tano
d. nne
2. Ni sentensi ipi iliyo sahihi?
a. Ajali ya Nakuru ndiyo iliyowaua abiria wengi
b. Idadi ya abiria wote waliofariki ni kumi no mmoja
c. Ajali ya Kiambu iliwaua abiria wanane
d. Ajali ya Garissa ilitokea karibu na kituo cha Tandu
3. Katika ajali ya kwanza ni watu wangapi waliokufia hospitalini?
a. Wawili
b. Hatujaambiwa
c. Sita
d. Wanane
4. Ajali ya lori ilitokea wakati upi?
a. Saa mbili jioni
b. Saa kumi na mbili asubuhi
c. Hakuna jibu
d. Saa thenashara jioni
5. Hospitali ya Nakuru iko katika jimbo lipi?
a. Uasin gishu
b. Kaskazini
c. Nakuru
d. pwani
6. walioumia pia wanaweza kuitwa
a. majeraha
b. wejeruhi
c. majeruhi
d. marehemu
7. neno mkahawa lina na maana gani?
a. Jingo la kuuzia chakula
b. Mti unaozaa kahawa
c. Jingo la kuuzia kahawa
d. Mahali ambapo watu hukaa
8. Kabla ya ajali zilizotajwa ni watu wangapi waliokuwa wamekufa kutokana na ajali mwaka huo?
a. Kumi na saba
b. Mia tano na sita
c. Mia nne themanini na kenda
d. Mia nne sabini na wawili
9. Ni nani aliyevunjika miguu
a. Utingo
b. Dereva
c. Mtoto
d. mjamzito
10. kichwa mwafaka cha habari hii ni
a. usafiri wa abiria
b. ajali wilayani
c. vifo vya watu
d. ajali barabarani

kiswahili revision papers