3.2. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 12:57 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Tangu nizaliwe sijapata kumwona mtu mwenye ukaidi kama Kazele. Lau kungekuwa na mashindano ya ukaidi ulumwenguni, basi Kazele angeongoza kwa medali yadhahabu. Hukuna siku aliyokubali nasaha, mapendekezo wala rai za wengine. Cnambilecho wahenga, ‘mwamba ngozi hunitia kwake.’ Siku ya arubaini ilipowadia, alijuta majuto ya Firauni ukaidi wake.
Siku hiyo ilikuwa jumatano mnamo saa kumi na mbili sa jioni. Ilikuwa ni siku ya soko. Kazele na sahibu yake Manono walikuwa wamepeleka kuku sokoni kuuza. Biashara haikuwa nzuri siku hiyo na hiyo ikawabidi wasubiri angalau wateja wa kununua hadi jioni. Hilo halikufaulu. Siku hiyo bahati haikuwa yao.
“Twende nyumbani ndugu yangu” Kazele alimwambia rafikiye.
“Wacha mchezo bwana we! Jua limeshakuchwa. Tutawezaje kupitia katikati mwa msitu ule mwenye ndovu saa hizi? Ni heri tutafute mahali hapa mjini tubwage mbavu zetu.’ Alimnahisi
“Mimi sipendi kuishi na watu waoga kama kunguru. Tufunge matenga yetu twende bwana” Kazele alimhimiza mwenzake. Manono alidindaakichelea mkosi wakati wa kupitia barabara ya pekee iliyopita mbuga ya wanyama.
Kazele alifunga tenga lake na kuwapanga vizuri kuku wake waliosalia kisha akapiga bismilahi na kuinukia baiskeli yake.
Alipokaribia msitu wa Dembwa giza lilikuwa limeula na kuumeza mchana. Kwa mbali kidogo, taa ya baiskeli yake ilimulika dubwana lililokuwa barabarani. Kazele alipokaribia alikumbana na ndovu akampigia kelele, akitaka ampishe njia. Mtume!kumbe sivyo! huo ulikuwa uchokozi wa hali isiyokadirika kwa hayawani huyo. Ndovu alirusha mkonga wake na kuikamata baiskeli kwa bahati nzuri Kazele alianguka chini. Baiskeli pamoja na tenga la kuku vilirushwa juu hewani, ungeiona baiskeli hiyo angani ungedhani ni eropleni ya tairi mbili. Kuku nao walitoka kwenye tenga na kutapakaza manyoya meupe mithili ya mvua ya theluji. Kazele naye alitundika guu begani
Kazele aliokoa roho yake kwa kuparamia mti mrefu hata hakutambua kwamba mti huo ulikuwa ma miiba kuanzia shinani hadi kileleni. Alibaki huko kileleni huku roho ikimtanga, jasho likimtoka na damu kumloa mwili mzima. Alikaa hali hiyo hadi macheo. Manono alipopita asubuhi hiyo, alipigwa na butwaa kuona manyoya ya kujku yametapakaa kote. Alianza kuomboleza. Mara akasikia sauti kutoka juu ya mti. “Niko hapa ndugu yangu.”
“Mti wote una miba, sijui nishuke vipi” aliinua kichwa na kumtazama Kazele. Alimtazama na kucheka kwa nguvu.
1. Maana nyingine ya neno ukaidi ni
a. Ujeuri
b. Uoga
c. Uongo
d. Uvivu
2. Kwa nini siku hiyo kuku hawakununuliwa
a. Hawakuwa wamerauka
b. Haikuwa siku yao
c. Hawakuwa na bahati
d. Ilikuwa jioni
3. Ukweli ni kwamba Manono alikuwa
a. Mwoga
b. Mtulivu
c. Anabusara
d. Ana ujasiri
4. Tubwage mbavu zetu ina maana ya
a. Tutulie
b. Tupumuwe
c. Tukae
d. Tulale
5. Ni jawabu lipi si sahihi msitu wa Dembwa
a. Unatisha
b. Una ndovu
c. Haupitiki kwa baiskeli
d. Unatidha usiku
6. Ndovu alikasirika
a. Aliposikia kengele
b. Alipomwona Kazele
c. Aliposikia baiskeli
d. Aliposikia sauti
7. Baiskeli ya Kazele
a. Iligeuka ndege
b. Haikuwa na taa
c. Ilitoka tairi
d. haikusalimika
8. Maneno ‘alipigwa na butwaa’ yana maana ya
a. Kuteseka
b. Kushangaa
c. Kuhuzunika
d. kuomboleza
9. kisa kinaonyesha kuwa
a. kuku walinusurika
b. Kazele hakunusurika
c. Kuku na Kazele walinusurika
d. Kazele alinusurika lakini kuku hawakunusurika
10. Funzo linalopatikana kutoka hadithi hii ni kwamba
a. Tusizingatie ushauri wa watu
b. Tuzingatie ushauri usiojaa
c. Tupende nasaha
d. Tupende ubishani

kiswahili revision papers