3.3. Kifungu cha Kujibu Maswali cha Tatu Sehemu ya Pili - Maswali

posted Jun 21, 2015, 9:17 PM by Maurice Nyamoti   [ updated Jul 25, 2015, 2:08 AM ]

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-10


Wale jamaa wakabaki pale wameduwaa wasijue la kufanya. Kujaribu kulikimbia jitu ni kazi bure kabisa. Wote walijiona ni watu wa kufa. Hapo Binta, kwa kuwa alikuwa mkuu wa familia, alipaswa kukata shauri haraka. Hakuwa na haya wala huruma za kumwambia mkewe achague kifunguamimba mmoja ampike. Mara kilio cha kulifungua mimba kilisikika. Nduguze nao walimwunga mkono katika kulia. Wote walifahamaki kinagananga kwamba kesho na keshokutwa, mtondo na mtondogoo na siku zifuatazo zitakuwa zamu zao.
Ingawa Binta alikuwa mwepesi wa kuchagua mtoto wake afe, lakini akili za mke wake ziliona vingine. Mkewe alifikiria jambo la kuwaokoa wanawe, haidhuru hata Bintu akifa. Akafanya maarifa na akamwambia mumewe,”kumwona mtoto wako akifasi vizuri. Vilevile watoto wetu kumwona ndugu yao akifa si vyema. Kwa hiyo nawaomba mwende mkachanje kuni na mtakuta mtoto huyu amekwishapikwa. Mimi lazima nibaki hapa ili nikafanye kazi za kupika.” Kwa bahati nzuri kama Yule alivyotaka. Wote walikubaliana naye. Kilio kikubwa kilifuata wakati ndugu walipokuwa wakingana na kaka yao mkubwa. Walipeana mikono ya buriani na kuahidiana kukutana wote pamoja huko peponi baada ya siku kumi na nane.
Baada ya kuondoka, mama alimwambia mtoto wake apande darini bila ya upinzani wowote. Mtoto akatii bila kukawia kasha mama alikiendea chumba kilichokuwa maiti ya watu waliokuwa wamekaushwa na Binta. Miili hiyo ilikuwa ya mashujaa waliofariki zamani ambayo Binta hakutaka izikwe. Aliubeba mwili mmoja akautumbukiza ndani ya pipa lichemkalo. Kisha akaliendea bohari la mfalme na kuchukua viungo vya kila aina. Akaanza kazi ya kuunfa mwili wa maiti. Mfalme na wanawe waliporudi, walidhani ni mmoja wao akitokota. Hakupenda hata kuangalia mwili wake au kuenda mahali pale wakisikia harufu ya marehemu.
Baada ya muda kupita, jitu lile liliwasili pamoja na fisi wake wawili. Lilipowahesabu watoto likaona jumla yao ni kumi na watatu. Lilipoangalia chunguni na kumwona maiti ikichemka, alikuwa na mengi ya kuulizia. Liliridhika kabisa. Kisha liliamuru nyama ipakuliwe. Ilipopea, fisi walifanya haramu yao. Mwisho jitu lilimwambia mama Yule afanye vivyo hivyo siku zote. Chakula lazima kiwe tayari kila siku kabla ya saa kumi alasiri. Kisha kuyasema hayo, liliondoka pamoja na fisi wale likaenda zake.

1. Watu hao hawakuweza kulikimbia jitu kwa kuwa
a. Jitu lina nguvu sana
b. Hawakuwa na pa kuenda
c. Binta alikuwa mkuu
d. Waliogopa
2. Kifunguamimba aliangua kilio kwa sababu
a. Alipigwa na jitu
b. Alichagiliwa kupikwa
c. Wenzake walimpenda
d. Nduguze wamwunga mkono
3. Mwandishi alisema kuwa Binta
a. Alimchagua
b. Hakutaka
c. Alifurahi
d. Alichukua
4. Watu hawa walipoagana buriani
a. Hawakutarajia kuonana tena
b. Walitamani kuonana tena
c. Waliahidiana kuonana
d. Walivunjika moyo
5. Mama alimwambia mtoto apande darini ili
a. Afe
b. Aliwe
c. Ajifiche
d. akalala
6. mama alipika maiti ya
a. mwanawe
b. Binta
c. Jitu
d. Shujaa
7. Jitu liliporudi
a. Lilimwona Binta akichemka
b. Liliuhudumia maiti ikichemka
c. Lilifurahia kifunguamimba kuchemka
d. Lilimpongeza mama
8. Jitu lile kisha
a. Liliuliza maswali
b. Halikutaka kula
c. Lilitaka kula
d. Lilipakua nyama
9. Liliamuru maana yake lilitoa
a. Umri
b. Hamri
c. Shauri
d. Amri
10. Habari hii inatuonyesha
a. Mama aliyetumia akili kuliko baba
b. Baba aliyeshinda mama kwa akili
c. Watoto walioliwa na jitu
d. Jitu lililowala watoto wa mtu

kiswahili revision papers